SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

09 October 2014

WATATU 'OUT' JESHI LA POLISI KAGERA

 Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewafukuza kazi askari polisi watatu kwa kosa la kukosa maadili mema ya jeshi la Polisi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Henry Mwaibambe,amewataja askari hiyo kuwa ni PC Asuma Mpaji Mwasumbi  mwenye namba F.7788,PC Fadhiri Linga mwenye namba G 2122 na PC Veronica Nazaremo Mdeme,wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Missenyi.

Akifafanua tukio hilo,Mwaibambe amesema askari hao walitenda kosa hulo la fedheha kwa kupiga picha kinyume na maadili ya jeshi hilo mnamo mwaka 2012 wakiwa kazini,picha ambazo zimesambazwa sehemu mbalimbali za mitandao ya kijamii hapa nchini. 
Alisema kuwa PC Fadhiri ndiye aliyehusika na kupiga picha hizo kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kuituma katka mitandao mbalimbali ya kijamii kitendo ambacho ni kinyume cha maadili kwa sababu mbalimbali. 
Amezitaja sababu hizo kuwa ni kupiga picha wakati wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha maadili ya jeshi hilo pamoja na kuituma picha hiyo kwenye mitandao mbalimbali. 
Aidha,Mwaibambe amekiri kuwa picha husika inayoonekana kwenye mitandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa,hivyo ni wazi kila askari kujua kuwa maadili ya kijeshi yapo kisheria na askari yeyote anafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la Polisi.

4 comment:

Anonymous said...

Jamani watumishi WA Una hasa polisi msidhalishe uniforms za jeshi bora mpige picha mkiwa uraiani

Anonymous said...

Pole kwao!

Prudence Karugendo said...

Ni kweli walisahau maadili au pengine hawafundishwi. Hayomavazi ni mali ya taifa, yanatakiwakulindwa na kuheshimiwa. Kufanya mambo yoyote machafu ukiwakwenye mavazi hayo nikulitukana taifa lako na wananchi wote

Hamshatz.blogsport.com said...

Wakike washonewe sare ndefu na pana zaidi wafiche maungo yao , hizi bado ni kulidhalilisha jesh na wanawake!

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU