Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisindikizwa na Daktari Bingwa Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya
Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji mwishoni
mwa wiki iliyopita.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana
na Daktari Edward Schaeffer muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka
katika hospitali ya Johns Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini
Marekani ambapo alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki iliyopita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo,
Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali
ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea
kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi
iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostate) na afya
yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.
Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza
kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini
kwenda kwenye Hoteli Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko karibu na hospitali hiyo.
Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa
matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya
uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete
atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya
matibabu yake.
Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo
amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu
ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni
+1-646-309-2295.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment