Bukobawadau

KUMBUKUMBU MABASI YA ABIRIA YA ZAMANI

Ndugu Wadau kwa wale walioenda Umri kidogo tunaweza kukumbushana mabasi yetu ya Zamani kwa kutoa Comment yako,jina la basi na Safari zake kipindi hicho mengi yalikuwa ni Leyland  au Tata .
 Enzi za Kabandole, Safari leo, Giligoli na Wenzake,Zaawayo,Tanganyika bus, compyuta mali ya Mzee Nassor harub wa  Kyabagenzi,Mshuti la Mzee Mathias wa Nshamba,Double Action mali ya Mzee Rubozi,Byaku -Kishanda hiyo,Kagera Retco ,Safari na Muziki , Mawingo Bus Service Ndugu yangu Salum Kapala na Vibweka vya Balimi kipindi hicho 'Bijabiwa',Rwabizi -Buganguzi , Kabeya na Fresh hapo kamachumu na nyinginezo kama Zawayo/Naba oyele jingine likiitwa Muungano wa vijiji Sheedah ilikuwa 'Abaimba na 'Kakwiki!!
Utaweza kuikumbuka 'Kabandole ' kwa wenzetu wa Kanyigo tunakumbuka "Morning Star Coach" jingine liliitwa Natabase Agaya  hapo unakutana  na konda maarufu sana bwana 'Bampalata vile vile kwa Wanakagera ilikuwabasi ya mzee KUGU'S maarufu kama kugis. ambayo baadae yalitaifishwa na operesheni uhujumi uchumi na kuundwa kampuni ya RETCO yote juu ya yote kwa wenzetu wa Ishozi mtakumbuka lile basi maarufu kama
 'RUGOYE'  mwisho ni lile Basi la BUJUGO likiendeshwa na mzee Festo Mhihuzi wa bujugo.
 Ni kumbukumbu ya Mabasi ya Abiria ya zamani tokea tupate Uhuru ,kwa Wana Kagera kupitia BUKOBAWADAU BLOG tunapata kukumbuka Ajali mbaya ambayo inaelezwa kuvunja rekodi ya matukio ya ajali ya barabarani ikuhusisha basi la 'SAFARI LEO' mali ya tajiri mmoja wa Katoke kwa jina Maarufu la Mzee 'Kibogoyo' hii ilitokea mwaka 1986 baada ya kupata tatizo la breki maeneo ya Amjuju-Kibeta .
Ingawa hatuna kumbukumbu sahihi ya Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo zaidi tunakumbuka Dreva wa Basi hilo aliitwa kwa jina la 'SHAKUBOTO' basi hilo likiwa Bibi Harusi aliyejulikana kwa jina la 'SABINA' tokea hapo tukapata msemo usemao 'Omkosi gwa Sabina' au Wagila Omkosi Nka Sabina.!!
Credit;Mc Baraka 
Next Post Previous Post
Bukobawadau