Utaweza kuikumbuka 'Kabandole ' kwa wenzetu wa Kanyigo tunakumbuka "Morning Star Coach" jingine liliitwa Natabase Agaya hapo unakutana na konda maarufu sana bwana 'Bampalata vile vile kwa Wanakagera ilikuwabasi ya mzee KUGU'S maarufu kama kugis. ambayo baadae yalitaifishwa na operesheni uhujumi uchumi na kuundwa kampuni ya RETCO yote juu ya yote kwa wenzetu wa Ishozi mtakumbuka lile basi maarufu kama
'RUGOYE' mwisho ni lile Basi la BUJUGO likiendeshwa na mzee Festo Mhihuzi wa bujugo.
Ni kumbukumbu ya Mabasi ya Abiria ya zamani tokea tupate Uhuru ,kwa Wana
Kagera kupitia BUKOBAWADAU BLOG tunapata kukumbuka Ajali mbaya ambayo
inaelezwa kuvunja rekodi ya matukio ya ajali ya barabarani ikuhusisha
basi la 'SAFARI LEO' mali ya tajiri mmoja wa Katoke kwa jina Maarufu la
Mzee 'Kibogoyo' hii ilitokea mwaka 1986 baada ya kupata tatizo la breki
maeneo ya Amjuju-Kibeta .'RUGOYE' mwisho ni lile Basi la BUJUGO likiendeshwa na mzee Festo Mhihuzi wa bujugo.
Ingawa hatuna kumbukumbu sahihi ya Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo zaidi tunakumbuka Dreva wa Basi hilo aliitwa kwa jina la 'SHAKUBOTO' basi hilo likiwa Bibi Harusi aliyejulikana kwa jina la 'SABINA' tokea hapo tukapata msemo usemao 'Omkosi gwa Sabina' au Wagila Omkosi Nka Sabina.!!
Credit;Mc Baraka
5 comment:
Byonabushai.Victor,Rehmuturah na Chipukizi
Ajali ya Safari leo ilikuwa 1984 nilikuwa natoka likizo ya uzazi na mwanangu alikuwa anaumwa lakini sikuweza kupata huduma sababu ya wingi wa majeruhi. I think it was in June.
Duh!! Unenikumbusha mbali mdau. Nimefurahi sana. Ila umekosea kidogo aina ya mabasi. Ni Leyland na Benz. Kipindi hicho Tata zilikuwa bado kabisa. Tata ni za juzi tu.. Asante mdau..
Dah ajali ya safar leo mteremko wa Hamugembe.Nilikuwa 14 years old!!
Yeah zilikuwa Leyland na Benz.Mabasi ya Tata yanafanana na mabasi ya Benz.Rubya kuna mzee Lugogo alikuwa nalo.
Post a Comment