Bukobawadau

MWILI WA MAREHEMU MTENSA LEONARD WASINDIKIZWA KWA HESHIMA KUBWA

 Hatimae mwili wa Marehemu Mtensa Leonard wasindikizwa na mamia ya watu wa rika zote kwa heshima kubwa ,tukio hili limedhihirisha Wema wake, upole wake,huungwana na namna alivyokuwa mtu wa watu kweli!!
'Sitoweza kusahau kwangu ni pigo kubwa sana Kwangu utabaki Kuwa baba nilikupenda na nitaendelea kukupenda Kataka maisha yangu I will always remember yo'...Ni maneno yake Bi Anitha Mtensa pichani
 Kutoka Chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya mkoa, mwili wa marehemu Mtensa uliwekwa juu ya Gari la wazi ambalo lilipita nje ya Klabu yake ya Lina's na kuzunguka kupitia Mtaa maarufu wa Jamhuri lilipo Soko Kuu la Bukoba. Maeneo yote ulikopitishwa mwili wa Mtensa, shughuli zote zilisimama na watu walidhihirisha kuwa katika majonzi makubwa kwa kuondokewa na Kamanda, muwekezaji ambaye Biashara zake zinahusika na kutoa ajira kwa watu wasiopungua Mia moja hapa mjini Bukoba.

 Uncle Majid Kichwabuta, akiwa imara kuhakikisha haki na heshima inayotakiwa kwa Marehemu Stivin Leonard Mtensa inapatikana.

Mji wa Bukoba na viunga vyake umeendelea kuzizima jioni ya leo kutokana na msiba huo, Katika hatua nyingine, vilio na simanzi vilitanda kila kona lilipopitishwa jeneza lenye mwili wake wa Marehemu Mutensa  Leonard.
 Mwili wa Marehemu Mtensa Leonard  ukiwa kwenye Gari  baada ya kuchukuliwa mochwari
 Taswira maeneo ya Mochari
 Vilio  vikiendelea kwa ndugu na jamaa wa kufuatia msiba huu
 Msafara wa Magari wakati ukikatiza barabara ya Uganda lilipo jengo la Linas Club
 Marehemu Mutensa  Leonard alikuwa ni mpambanaji aliyejitahidi kuibadilisha Bukoba kwa jitihada za ujasitiamali. Ni miongoni mwa wazaliwa wa Bukoba ambao kwao Bukoba ilikuwa ni kila kitu, kuwekeza Bukoba kuna changamoto nyingi. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake litukuzwe. Tumuombe Mungu aipokee roho ya marehemu na ampatie pumziko la amani.
 Muendelezo wa matukio kupitia Bukobwadau Blog tupo Uganda Road lilipo Jengo la Ukumbi wa linas Club.
 Maeneo ya Soko kuu hali ilikuwa hivi
Usawa wa daraja la Hamugembe.
 Hakika ni hali isiyoweza kuelezeka.
 Umakini mkubwa , Upendo wa kweli hakika kaka Mkuu E. Nyambo ni mfano wa kuigwa

 Kushoto ni Mjane wa Marehemu Mtensa Leonard, Mama Lina akiongozwa na Bi Jeanifer
Simanzi ,majonzi na huzuni mkubwa kwa familia ya Marehemu Mtensa Leonard.
Muongozaji wa shughuli nzima kwa jioni ya leo ni Mc Lutakwa pichani.
 Gari lenye Mwili wa Marehemu Mtensa Leonard linawasili nyimbani kwake Kyakailabwa.


 Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi Ndg Self Super Mkude akitoa utaratibu
 Mzee Super Self Mkude anashindwa kuendelea... na kutokwa na machozi ya uchungu!
 Baada ya Mwenyekiti wa kamati ya msiba huu Ndugu Self Mkude kushindwa kuongea  ikabidi asaidiwe na Kaka Mkubwa E. Nyambo pichani akiendelea kutoa taratibu.
Ibada fupi ya kuuombea mbili wa Marehemu Mtensa ikiendelea.
 Hakika ni Simanzi kwa kila mtu.
 Ndugu Peter Matete akiwa na uzuni mkubwa
 Mama Edan/ Rugalabamu akimfariji Ndg Peter Mgisha.
Wadau mbalimbali katika sintofahamu kufuatia msiba huu mkubwa.
Sehemu ya ndani wapo kinamama  wengi tu.
 Ndugu Kilaja pichani kushoto
Katikati ni Mtoto Mkubwa wa kuzaliwa na Marehemu Mtensa , Ms Linas.
 Kutoka kushoto  Ndg Rahym, Gsmart George, E. Nyambo , Ndg Mwinyi na Mr Pajero
Wanaonekana watoto wa Marehemu Mtensa Leonard pichani
Taswira mbalimbali eneo la tukio ikiwa sehemu kubwa ya wadau wameusindikiza mwili wa Marehemu Mtensa
Bi Asia na Bi Jeannifer.
Mdau Frances na Ndugu George
Kwa matukio zaidi ya picha Ingia hapa>Bukobawadau Entertainment Media

Next Post Previous Post
Bukobawadau