Askari
wa Magereza akimfungua pingu Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu
Tanzania leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu., ambapo leo yeye na
wenzie 49 wameachiwa huru ila watatumikia kifungo cha nje cha mwaka
mmoja. PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
HATIMAYE
katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa
Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote
yaliyokuwa yakiwakibili.
Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja
kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara
baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka shangwe za
furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na
eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja
na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo
mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama
hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na
masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua
kuna tatizo umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu
awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai
mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande
wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya
mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu
za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni
yaliyokusudiwa.
Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda baada ya kuachiwa.
Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
Wafuasi wa Sheik Ponda wakimshangilia alipokuwa akihutubia ndani ya Msikiti wa Mtambani.
Katibu
wa Jumuia za Taasisi za Kiisalamu Tanznania, Sheikh Ponda Issa Ponda
akifanya mahubiri katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam,
alipokwenda leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia
huru jana, yeye na wenzake 49 waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la
uchochezi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment