WAZIRI MUHONGO(UTETEZI WA SERIKALI)
Anaomba radhi kama jana kulikuwa na usumbufu wa umeme na anawaagiza mameneja wote wa TANESCO wasikate umeme.
Anatoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow, mengi yamesemwa na ni wakati wa
kuanza mjadala kujua ukweli, Shukraan kwa CAG, TAKUKURU na PCCB kwa
uchunguzi. Pia nawashukuru PAC, jana tulitulia kuwasikiliza PAC na leo
tutulie tusikilize utetezi wangu.
Miaka ya 90 tulikuwa tuna upungufu wa umeme kutokana na maji, 1994
serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa inamiliwa na VIP ya
Tanzania iliyokuwa na 30% na Mechmar ya Malaysia 70%.
Kulingana na Mkataba wa PPA kati ya TANESCO na IPTL, majukumu ya IPTL
yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha (Build, Own and Operate –
BOO). Hivyo, kutaifisha Mtambo huo ni kukiuka makubaliano katika Mkataba
wa PPA wa tarehe 26 Mei 1995, ukiukwaji wa aina hii ukitokea unaweza
kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa ni pamoja na kushtakiwa
kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa. Aidha utaifishaji wa miradi
ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya kufukuza wawekezaji binafsi
Kwa mujibu wa Mkataba huo, IPTL ilitakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua Asilimia 85 ya uwezo wa Mtambo.
Hata hivyo, uzalishaji wa umeme haukuanza mara moja kutokana na mgogoro
uliotokea kati ya TANESCO na IPTL kuhusu gharama halisi za uwekezaji na
namna ya kukokotoa Capacity Charges. Hivyo, IPTL ilianza kuzalisha umeme
tarehe 15 Januari, 2002. Kutokana na hali hiyo muda wa miaka 20 ya
Mkataba ulianza kuhesabiwa tarehe 15 Januari, 2002 baada ya kuanza
uzalishaji (Commercial Operation Date).
Migogoro kati ya TANESCO na IPTL ilianza muda mfupi baada ya PPA
kusainiwa tarehe 26 Mei, 1995. IPTL waliitaka TANESCO wakubaliane bei za
kununua umeme kwa kuzingatia gharama za uwekezaji. Pande hizo mbili
zilishindwa kukubaliana gharama za Capacity Charge kwa vile TANESCO
walidai kuwa gharama zilizoainishwa na IPTL ni kubwa kuliko gharama
halisi za uwekezaji. Mwaka 1998, TANESCO iliajiri Kampuni ya Mawakili ya
Mkono & Co. Advocates kutoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na
Huntons & Williams ya Marekani. Kutokana na tofauti za gharama za
Uwekezaji, Mawakili hawa waliishauri TANESCO ifungue Kesi ICSID nchini
Uingereza dhidi ya IPTL ili kupinga gharama hizo.
2004 TANESCO ilifungua shauri kupinga tozo la capacity charge
Taarifa hio sio kweli kwani TANESCO haijawahi kufungua kesi yoyote dhidi
ya standard charted kama ilivyosemwa na PAC. Kesi hiyo ilifunguliwa na
Standard charted na ilikuwa haihusu capacity charge. Hamna kokote
mkataba kati ya standard charted na TANESCO.
Makinda ameingilia na kusema ripoti itatolewa baada ya wabunge kudai ripoti.
Muhongo anaendelea
Ukweli ni kwamba kutokana na maamuzi ya ICSID 1 ya tarehe 12 Julai,
2001, gharama za ujenzi wa Mtambo wa Tegeta ni Dola za Marekani 127.20
kama ilivyoelezwa katika Ukurasa wa 47 Aya ya 4 ya Taarifa ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Katika Taarifa hiyo, pia
imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano wa deni na mtaji utakuwa 70:30.
Hii ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za Marekani milioni 89.04 na
mtaji ni Dola za Marekani milioni 38.16. Uamuzi huo haujabadilishwa na
Mahakama yo yote au mtu ye yote.
2004 kampuni ya Mkono and CO advocates iliishauri TANESCO iendelee kupinga capacity charge ICSID (International
Centre for Settlement of Investment Disputes) London. Hata hivyo
haikuishauri TANESCO kufungua kesi za katika mahakama za Tanzania wala
mahakama ya kimataifa. Hadi 2013 jaji Utamwa anatoa hukumu ya mgogoro wa
wanahisa wa IPTL kulikuwa hamna kesi yoyote kuhusu tozo ya IPTL.
UUZAJI WA HISA ZA VIP
Kutokana na kutokubalina Mechmar iliishauri VIP ifungue
shauri. VIP ilifungua shauri Tanzania ikiomba IPTL ifilisiwe. Uamuzi
ulitolewa kwa shauri la VIP. Chini ya Kimario, alipewa mfilisi wa mda
kulinda mali za IPTL, kufanya uchunguzi ili mahakama iweze kutoa uamuzi.
Uamuzi ulitoka baadae, IPTL iwekwe kwenye ufilisi kamili chini ya RITA.
Hukumu ilipingwa mahakama ya rufaa ikianisha dosari katika uamuzi wa
mahakama kuu na Standard charted Hong Kong. Mahakama ya rufaa
ilikubaliana na hoja hiyo na ilipelekwa tena kwa mfilisi wa muda
kukusanya madeni, kusuluhisha mogogoro na kuendesha mitambo ya IPTL kwa
niaba ya IPTL.
Serikali haiwajibiki kuingilia hisa za makampuni binafsi, mauzo ya hisa
yaliyofanyika nje ya nchi yatatambuliwa tu endapo yatatambuliwa na
BRELA. Uhamishaji wa hisa 7 ulisajiliwa hapa nchini. Kamati katika
uthibitisho huo inakubali hisa za Mechmarr zinamilikiwa na PAP
Hiza saba za IPTL zinatambuliwa pia na Standard Charted, Kama PAP
haimiliki asilimia sabini kwanini wana makubaliano na standard charted
ya Uingereza.
Ilifilisiwa Malaysia na sio Tanzania, madai ya standard charted dhidi ya
TANESCO ni kwa sababu IPTL waliweka dhamana mtambo wa kuzalishia umeme,
Lakini benki ya Hong Kong ilikosa sifa ya kufungua shauri Tanzania
hivyo ilifungulia Uingereza
VIP chini ya usuluhishi wa RITA iliuza hisa zake PAP kwa dola milioni 70
na ndivyo ilivyomaliza mgogoro wa IPTL. Mimi sio dalali wa hii biashara
bali ni dalali wa(anasema mambo mazuri aliyoyafanya kama kusambaza
umeme vijijini)
Makinda amekuwa mkali kidogo kwa Muhongo asome taarifa na asiseme ambayo hayamo.
ESCROW ACCOUNT
TANESCO kwa ushauri wa mkono walitoa hoja kuwa gharama za kununua umeme
na makadirio ya mtaji walitoa notisi(invoice disputes notice) ya kupinga
usahihi wa malipo. Alietoa ushauri ni kampuni ya Mkono, 2006 serikali
ulisaini mkataba wa kufungua account ya Escrow.
MMILIKI WA FEDHA YA ESCROW
Account ya Escrow ilipaswa kuwa na bilioni 306 zilizowekwa na TANESCO.
PAC walitoa mapendekezo kuwa imethibitisha kuwa mchakato wa kutoa pesa
Escrow umegubikwa na mchezo mchafu na kutakatishwa na benki mbili nchini
TAHADHARI ZILIZOCHUKULIWA
Serikali ilichukua kinga kutoka IPTL, kwa mujibu wa kinga IPTL
itawajibika yakitokea madai yoyote na ilipitiwa na mwanasheria mkuu wa
serikali. (Yoyote anaedai chochote aende IPTL)
PAC wameeleza serikali haikuchukua tahadhari ya kutosha juu ya madai mapya kama yangejitokeza kitu ambacho sio kweli.
DHANA YA MADAI YA BILIONI 321
Madai kwamba TANESCO inaidai IPTL 321 Bilioni, bodi ya TANESCO imekana
kuyatambua madai haya na vitabu vya TANESCO vinavyokaguliwa na CAG
hakionyeshi madai haya.
Madai yaliyowasilishwa na mufilisi, yalitakiwa kuhakikiwa lakini hayakuhakikiwa na hayakuwa na uhalali wowote.
Kamati ya PAC, wamesema yana uhalali japo uhalali wake unategemea maamuzi.
TANESCO kwa kushirikiana na IPTL ilifanya uhakiki ili kujua madai halali
ya IPTL kabla ya kufanya malipo. Deni la TANESCO kama capacity charge
lilikuwa $370milioni ambazo ni pungufu ya $90 milioni ya madai ya IPTL.
Yalifanyika hoteli ya Kunduchi na majina ya waliokuwepo anawataja.
Hizi takwimu zinaonyesha hakuna fedha yetu pale tunayodai bali tunadaiwa
na IPTL. Hamna fedha ya umma popote bali tunadaiwa na makampuni ya
uzalishaji umeme(anataja makampuni na madeni wanayodai).
Madai yoyote yaliyotokea nje ya nchi laima yasajiliwa nchini, shauri la London haliusiani na fedha za IPTL.
Madai dhidi ya IPTL ikiwemo VAT, serikali ilitaka kinga.
Gharama za mawakili za Mkono adv, hadi hukumu inatoka 2013. TANESCO
na serikali zililipa mawakili bilioni 62.9 na bado mawakili hawa wanadai
TANESCO $ milioni 4.5 na walipendekeza wapewe kazi nyingine ya kwenda
kupinga huku lakini bodi ilikataa kuendelea na hio kazi. Tunajua fika
tumepata hasara gani kupitia kampuni ya Mkono.
Kumalizika kwa mgororo na IPTL tumeokoa bilioni 95 za uwakili. TANESCO
ilikua na nafasi finyu mno ya kushinda kesi ya London kulingana na
ushauri wa mawakili ushauri unaogongana.
2013 kwa mujibu wa RITA, IPTL ilikuwa inaidai TANESCO $224.3 milioni, taarifa ya CAG inasema fedha za Escrow ni za umma.
FEDHA SIO ZA UMMA
TANESCO ilisimamisha malipo ya Escrow na ya IPTL kuanzia mwaka 2010 japo iliendelea kupata huduma kadri ilivyohitaji.
Hakuna fedha ya umma Escrow
Account ya Escrow iilikuwa na 182 na bado kuna upungufu wa 122 katika deni la IPTL.
Kamati haikupitia majukumu ya wazira, Mikutano ya bodi wakurugenzi
TANESCO, PAC inasema ilifanya mikutano miwili mfuulizo hivyo kutia
shaka. Si sahihi bodi ya TANESCO ilikuwa na njama.
Hoja ya mwanasheria wa TANESCO kazi, Taarifa ya PAC inasema mwanasheria
iliagizwa kwenda Malashia na aliporudi kuwasilisha ripoti ya due
deligence aliachishwa kazi.
Mwanasheria wa TANESCO aliomba kwenda Malasia kwa madai kuwa alipewa na
mwanasheria mkuu wa serikali kitu ambacho ni uongo na aliomba kuacha
kazi mwenyewe kwa kutoa taarifa kwa mkurugenzi mtendaji.
Alisema anaacha kazi kwa hiari yake mwenyewe kufanya shughuli zake binafsi. Hivyo bodi haikuwahi kumfukuza huyo mfanyakazi.
Hii kesi mimi nilielezwa na bahati mbaya bodi haikufata ushauri wangu wa kumshitaki muhusika.
WABUNGE WANADAI NAKALA YA RIPOTI KWA NGUVU NA BAADHI KUMUITA MWIZI
Anamalizia hapa kwa nukuu(anazinukuu nukuu kwa kiingereza na tafsiri zake), Spika anamwambia amalizie.
Spika amesimama tena kupoza hali ya hewa, Anamlazimisha waziri amalizie.
Waziri anawasilisha hoja na kumaliza.
MATANGAZO YA KAZI
Shughuli za bunge zimesitishwa mpaka saa kumi na moja.
KWA MAELEZO ZAIDI GONGA HAPA UPATE KUDOWNLOAD KIAMBATANISHI HUSIKA
KIKAO CHA BUNGE JIONI
Lissu: Anaomba radhi ya kauli ya jana kuhusu tuhuma ya wakili kumuua mkewe.
Escrow: Muhongo kapotosha, viambatanisho haviwakilishi alivyosema.
Muhongo ameleta vitu viwili tofauti na ni upotoshaji mtupu. Pesa za
Escrow ni za umma au binafsi, Muhongo anasema ni za makampuni na PAC
inasema ni pesa za umma. Isingekuwa za umma amri ya kutolewa
zisigetolewa kwa ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali.
Benno Ndulu asingesema siwezi kutoa bila ridhaa ya waziri mkuu na raisi,
pesa za binafsi iweje zitolewe kwa mlolongo wa mawaziri,
Ili PAP wapate pesa ilikuwa lazima wapate ridhaa ya Muhongo lakini hawajapa.
Nyaraka zinathibitisha mgao wa hizi fedha, zimepelekwa benki binafsi na
ndani ya siku moja baadhi ya watendaji wa serikali wamelipwa.
Mgao wa fedha za Escrow kwa maafisa wa umma, maaskofu na wabunge ndani ya siku 1 (bilioni 78); ni pesa za umma.
Mpaka majaji wamehongwa milioni 400 eti michango ya harusi!
Hizi fedha ni fedha za wananchi wa nchi hii! Kuna ushahidi wa kutosha katika ripoti ya PAC (TRA, CAG wamekiri)
Lazima watu wawajibike! Hizi ni fedha za Umma
Kumwondoa rahisi ni vigumu kidogo. Tuanze na Waziri Mkuu, Muhongo, Tibaijuka, Werema na majizi yote! Hawa tunawaweza
Mahakama zetu katika hili hazina mamlaka ktk kesi hii ya IPTL
Kwa ushahidi huu, ni ngumu kuwaamini majaji wetu na mahakama zetu
Kuna mawasiliano lukuki kati ya Ofisi za Umma katika utoaji wa fedha za Escrow. Haziwezi kuwa fedha binafsi
Fedha hazikutakiwa kutolewa na benki na haiwezi kufundishwa kazi na
mwanasheria mkuu, Chombo pekee cha kutoa ushauri wa kodi ni TRA na sio
mwanasheria mkuu na katibu mkuu wa fedha hawezi kujificha nyuma ya
kivuli cha ushauri wa mwanasheria mkuu.
Waliokuwa na mamlaka hawakufanya hivyo lazima wawajibike.
Waziri mkuu anatakiwa awajibike kwa sababu alikua anafahamu juu ya hili
swali, na barua zote zilinakiliwa kwa waziri mkuu, ni kiongezi
anaeshughulikia shughuli za kila siku za serikali.
Usalama wa taifa na financial inteligence unit chini ya wizara ya fedha hawakutimiza wajibu wao nao hatuwezi kuwaacha.
Waziri wa nchi ofisi ya Raisi(Marry Nagu) amesimama kuelezea
kutajwa raisi katika kashfa, anaomba watu wajadili kwa ustaarabu kufika
maamuzi pia kutotumia majina ya majaji.
Mwenyekiti amesimama na kusema anakubaliana nae pia anaomba watu wasitumie vijembe
Lissu: Anakana kutumia jina la raisi kwa dhihaka, na anarudia
aliyoyasema. Wazuri kupewa hongo ni jambo baya, pia mwanasheria mkuu wa
zamani kupewa hongo pia viongozi wa dini na inafedhehesha taifa. Hakimu
kupewa milioni 400 na kampuni ambayo ilikua mahakamani 20. Jambo baya
fedha za serikali kuibiwa. (Anataka kuongolea Mkono Adv lakini kengele
inagonga na kukaa chini)
Mwijage: Naijua IPTL tangu inaanza na imekua ni tatizo, hiki
kibuyu kilianza kula njiwa mpaka kula mbuzi kama alivyonisimulia bibi
yangu, IPTL imekua jini, badala ya kuhamaki tutafute njia ya kuondokana
nahiki kibuyu.
Tatizo mojawapo wa IPTL ni capacity charge kama nilivyoona kwenye hukumu
ya IPTL, Wananchi wamechanganyikiwa na kila unachomwambia kama madawa
na madawati anakwambia Escrow. Nakubaliana na PAC ilatudadavue wote
tutoke na maazimio ya pamoja.
Kingwangala anaomba taarifa: Taarifa kwa mchangiaji, PAC imefanyia kazi
ya CAG, hivyo findings za PAC zinatokana na CAG. Hivyo wachingiaji
wasinukuu sana taarifa PAC badala yake watumie taarifa ya CAG.
Mwijage anaendelea
Naomba wananchi waambiwe ukweli, watu wanapendekeza tubinafsishe mtambo
wa IPTL lakini tuwe waangalifu, tunaweza kujikuta tunabeba deni la
standard charted, hatuwezi kuingia ndoa na standard charted bank.
VAT, Ile pesa ya VAT, tunataka kujua mmedai kiasi gani.
Kuna watu wamechukua pesa, Rugemarira alisema tunalaliwa, Isiwe nongwa yeye kulipwa hizo pesa.
Nani aondoke, sioni tatizo kumsema waziri wa uingereza, hivyo
waziri Masele sidhani kama ana cha kuwajibishwa, sioni waziri mkuu
amehusika wapi. Kuna mtu ni halali, Mhongo ni dalali, huwezi kuwa waziri
wa umeme usikutane na mwekezaji wa Megawats 500. Tukaze pale
panapohusika, tumefika katika hatua mbaya.
Mohammed Chombo: Kama waliotangulia kusema, pia baada ya kupata
ripoti na ufafanuzi wa serikali, nami nichangie nililoliona, Escrow ni
account iliyofunguliwa baina ya watu wawili. Ilibidi ifunguliwe kwa
sababu ya kutoelewana kwa malipo yanayopaswa kulipwa.
Mwenyekiti(Zungu) anaomba order(utulivu wa bunge) kusikiliza anachoongea Chombo.
Chombo anaendelea
IPTL ni ushirika wa watu wawili na mmoja wao ni VIP na ikafika wakati
wakafungua kesi(anaendelea kuelezea historia ya IPTL na TANESCO),
Anatumia neno kuwakejeli wote wanaompinga/ kumpigia kelele
Fedha hizi sio mali ya umma bali ni mali ya IPTL, kama kuna pesa au kodi
ni lazima ilipwe na waliopata pesa hizo mfano VIP. Kwa fedha ambazo
zimebaki kwa PAP pia lazima zilipiwe kodi. Mimi sikupata pesa za IPTL.
Mwenyekiti(Zungu) anasema amemuona Lema anaropoka na anamkanya kama onyo la mwisho
Mheshimiwa nashukuru kwa kunipa nafasi(Amemaliza)
Mfutakamba: Usajili wa IPTL jukumu lake ni BRELA, anaepata hisa
hizo ni tax agent na anapaswa kwenda kulipa kodi, bilioni 30 ambazo
hazijalipwa kodi waende wakalipe kwasababu tunazihitaji.
Kama kuna mgao wa pesa umetolewa ni income hata kama ni zawadi lazima
walipe kodi, ningeshauri wale waliopata mgao walipe kodi. Ningependekeza
tujue hizi ni kesi za Britain zilikuwa ni kesi gani na kama PAP
alisajili Tanzania, bado naona utata kama PAP imesajiliwa Tanzania iweje
iwe kampuni fake.
Huu mradi ulikua gharama yake ilikuwa juu ya kawaida (overpriced), pesa
zilikua mali ya TANESCO lakini IPTL ilendelea kuzalisha umeme na bado
tunadaiwa. Kuna kampuni nyingi zinazalisha umeme hivyo tusije kuingizwa
mtego wa malengo ya kibiashara ya wazalisha umeme.
Nampongeza Muhongo na wizara yake kwa kutuletea umeme wa kutosha.
Tuangalie vielelezo vya PAC kama kuna watendaji katika utendaji wao kuna
hitilafu na sisi tuone.
Kuna wabunge wanatajwa kuwa wamepokea mgao, tuwape natural justice ya
kuwasikiliza. Tujue na wao sababu yao. Waliotajwa wapewe fursa wahojiwe.
Rugemarira amelipa kodi baada ya kulipwa. Waziri mkuu ni mchapakazi.
Makani: Nashukuru kwa fursa, tumeingia kwenye hoja inayohitaji
umakini mkubwa, ili tuweze kwenda vizuri lazima tumuweke Mungu mbele na
ili tumuweke mbele hatuwezi kuweka amabyo yanamuuzi kama uwongo. Hoja
inayonikira ni kuwa kuna fedha za serikali zilikuwa sehemu na baadae
ikaibwa na kuporwa. Wataalamu watusaidia kulingana na taaluma zao na kwa
kufuata maadili ya taaluma zao. Hoja kuu kama fedha ni za serikali ama
laa.
PAC wanakiri sio fedha zote za Escrow ni za umma, katika majibu ya CAG
hakuna mahali alipokiri kuwa fedha hizi ni za umma. TAKUKURU ilipohujiwa
na PAC amesema ni fedha za serikali japo hajakamilisha uchunguzi,
zingeweza kuwa fedha za serikali kama TANESCO wangerudi kwenye meza na
IPTL na majibu yakawa chanya, pili labda suala la kodi.
Si sahihi ukisema moja kwa moja kuwa ni fedha za serikali, majadiliano
kati ya TANESCO na IPTL, hata ukifanya mahesabu, pesa za escrow zote
zingezama katika deni la IPTL wanaloidai TANESCO.
Maoni yangu: Taarifa ya CAG ilikua na mapendekezo, yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na PAC(Anataja mifano ya tofauti). NASHUKURU
ZITTO: Anaomba muongozo juu ya muongeaji aliyepita kuhusu CAG hakusema fedha za Escrow za nani.
Ndasa: Muhimili mmoja kuwa na mgogoro na mwingine haileti sifa
nzuri hivyo kila mtu aheshimu muhimili mwingine, wananchi wanaposikia
kuna wizi, tusipoeleza vizuri hata tukiongea vipi humu haitasaidia.
Wananchi wanataka kujua ni kweli hizi pesa zimeibiwa au zimelipwa. Umeme
lazima ulipiwe IPTL kwa sababu hamna cha bure pale. Bilioni 320
zimeibiwa au zimetumika kulipia umeme? Katika hizi 320 bilioni pia
ielezwe kodi ya serikali ni kiasi gani. Wakija mafundi wa kusema
wananchi wataaminishwa kuwa ni wizi hivyo serikali lazima iseme bila
kuficha na msiwe na kigugumizi.
Tunamuwajibisha waziri mkuu kwa kosa lipi, tutendeane haki, mtoto wa
mkulima amefanya nini? Pili wametajwa watendaje kama Muhongo na Masele,
kwenye haki tusiweke ushabiki kisa Muhongo amekutana na Rugemelira
pamoja na Singh.
Kumezuka mtindo wa kusingizia watu, nafsi ya mtu itamsuta,
tusisingiziane. Namshukuru Zitto ni msikivu, PAC ni kamati ya bunge,
tushirikiane tutoe mapendekezo ya pamoja.
Tuwe makini tunavyoenda, kuna mataifa ya nje kama tukiwapa moyo hawa
tutaanza kuuza umeme nje, kuna bomba la gesi limekamilika ndani ya mwaka
mmoja.
Kisangi: Asante, nimpongeze Ndasa kuliweka jambo vizuri kama
wanakati wa nishati. Ntaanza na hitimisho la kamati ya PAC. Sikubaliani
na mapendekezo ya PAC. Sioni waziri mkuu amehusiki vipi pia serikali
wametoa majibu yanayoeleweka. Mapendekezo ya kumuondoa waziri wa
nishati, wapi Prof amehusika? Katibu wa nishati wapi amehusika? Tuache
chuki! Tusiandalia sura tuangalie wamefanya nini! Katika wizara
iliyofanya kazi ni nishati na madini. Huo ulikuwa utangulizi.
Taarifa(Mpina): Taarifa ya PAC si taarifa ya upinzani hivyo kusema ina njama za upinzani sio kweli.
Kisangi anandelea:
TANESCO ina madeni ambayo hata ukichukua pesa za Escrow inabaki
sifuri, mizania ya TANESCO inaonekana kuna madeni, mtu ukikosa kupata
haki yako unakimbilia mahakamani,
Taarifa Lugola: Isingewezeka kwenda mahakamani kwa sababu mkataba ulisema waende ICSD kukitokea mgogoro
Kodi mnayosema haiwezi kufatwa kwa sababu mwanasheria mkuu wa serikali alishatoa msamaha
Kafulila: Hasara ya jambo hili sio bilioni 320 pekee, mwezi wa
tisa mwaka huu ulikuwa ndio USA inasaini makubaliano ya MCC sehemu ya
pili lakini kutokana na kashfa hii hadi sasa haijasainiwa,
Taarifa(Muhongo): Tanzania inaendelea vizuri kuhusu MCC
Taarifa(Saada Mkuya): Si kweli September bali December MCC inakaa kwa ajili ya kupitisha hivyo bado hatujafika huko.
Taarifa(Nassari): Muhongo amedanganya Bunge kuhusu Masele, hajawahi kuteuliwa kuwakilisha vijana.
Kafulila: Hasara tuliyopata ni zaidi pesa za Escrow, hasara ya
kwanza ni MCC, hasara ya pili nchi wahisani kupitia bajeti wamegomea $
milioni 500. Katika MCC 1/3 ilikuwa miradi ya umeme lakini tumepoteza.
Barua ya Mramba(mgurugenzi wa tanesco) aliomba muda kupiga mahesabu ya
overcharge ya TANESCO ambapo waziri kaja kulidanganya bunge.
Zitto(Taarifa): Mkopo kwa ajili ya IPTL una Gvt gurantee, na nazungumza kama authority on this.
Leizer: Tuvunje taarifa zinatupotezea muda
Mwenyekiti: Hakuna taarifa tena
Kafulila: Kwenye hoja hii, fedha ni za umma au IPTL? Tukumbushane
waziri wa nishati wa madini alikua akisisitiza kuwa fedha zilitolewa
kwa hukumu ya jaji Utamwa, nilivyohoji nikaiwa Tumbili. Hukumu hii hapa
na hamna sehema iliyosema fedha hizi ni za Escrow, leo anasema ni kikao
cha Kunduchi beach na si hukumu. Hatusemi hawana mazuri waliyoyafanya
lakini kwenye wizi hukumu iko pale pale. Hawa jamaa wamekula pesa za
Escrow pamoja za VAT, madalali wa wizara ya nishati wamesababisha hasara
zaidi ya mramba ya bilioni 11 lakini leo yuko mahakamani
London walisema fedha za overcharge zirejeshwe lakini mtu ambae hukumu
iko kwa manufaa eti ndo anagoma kutekeleza(comply). Kama Seth
alivyoangusha TANU Kenya ndivyo atavyoiangusha CCM Tanzania.
Transfer of shares ikifanyika waziri wa sekta husika lakini waziri
anasema kampuni binafsi serikali haingilii. Imefika mahala tuwajibika,
tunaposema waziri mkuu awajibike(MUDA UMEKWISHA)
Lusinde: Jambo hili tangu tumeanza kulijdaili, limeingiliwa na makundi kama manne hivi;
1. Waliopata
2. Waliokosa
3. Wanaotaka urais
4. Mawakili na Mabenki
Lusinde: tukiendelea kuchangia kwa kufuata makundi hayo tutakuwa hatufiki popote.
Lusinde: Mnasema fedha sio serikali sasa kama fedha sio za serikali tangu lini CAG akakagua fedha zisizokuwa za serikali.
Lusinde: Watu waliopokea mimi sina shida nao ila nina shida na fedha zilipotoka huko nyuma, zimetoka wapi?
Lusinde: Siasa haina urafiki wala uadui wa kudumu, jana Zittokabwe wakati anawasilisha ripoti naona Mbowe anampigia makofi.
Lusinde: Waziri mkuu katangaza nia ya Urais kimya kimya basi na sisi tumpige kimya kimya maana sijaona sehemu aliyotajwa.
lusinde: tusitangulize chuki kwa sababu umekosa. viongozi wa dini
hupokea sadaka wasizozifahamu. tusiwahoji bali tuhoji zilipotoka.
Lusinde: tukiendelea kuchangia kwa kufuata makundi hayo tutakuwa hatufiki popote. #TegetaEscrow
lusinde: Mnasema fedha sio serikali sasa kama fedha sio za serikali tangu lini CAG akakagua fedha zisizokuwa za serikali.
Lusinde: Watu waliopokea mimi sina shida nao ila nina shida na fedha zilipotoka huko nyuma, zimetoka wapi?
Lusinde: Siasa haina urafiki wala uadui wa kudumu, jana Zittokabwe wakati anawasilisha ripoti naona Mbowe anampigia makofi.
Lusinde: Waziri mkuu katangaza nia ya Urais kimya kimya basi na sisi tumpige kimya kimya maana sijaona sehemu aliyotajwa.
Lusinde: Zitto Kabwe ulipokea fedha kutoka sehemu mbalimbali ukitumia watu tofauti, leo inabidi utupe majibu yako.
Lusinde: Leo mnasimama hapa awajibike awajibike, wewe umewahi kuwajibika? unadhani kuwjaibika mchezo?
Lusinde: Mzee Pinda we nenda na kimya kimya yako hadi Mungu atakapokujalia. Habari ya kukutoa hapa haipo.
Mhe Dk Hamis Kigwangallah anatoa taarifa;
DK Kigwangwalah: Kamati ya PAC ni kamati amabyo wajumbe wake wanatokana na Bunge hili.
Dk Kigwangalah: Kusema watu wote wangeitwa kuhojiwa tusingeleta taarifa kwa wakati tulichofanya ni kusoma mahojiano yao na CAG.
Mbowe: Ni vyema tukatenda haki, katika taarifa ya Muhongo
alimzungumzia Ngwilimi(Ananukuu alivyosema ikiwemo aliamua kuacha kazi
mwenyewe baada ya kudanganya ametumwa Malaysia na mwanasheria mkuu).
Hizi taarifa sio za kweli na taarifa za kumtuma Malaysia alitumwa na
mwanasheria mkuu wa serikali na anaonyesha barua.
Muongozo(Masele): Ningependa muheshimiwa atuonyeshe kama imenakiliwa TANESCO.
Mbowe: Ni aibu naibu waziri kumkana mwanasheria mkuu wa serikali,
napenda kushauri taifa, tunanyukana bila sababu za msingi. Kubwa ni
kujua ni fedha za umma au za watu binafsi. Haiwezekani kuchukuliwa
kinyume za taratibu hata kama sio za serikali. Hii miamala yote
iliyofanyika ni halali?
Tunapofanya maamuzi tuwe makini yasije kuturudia siku zijazo kama Richmond, waziri mkuu anatakiwa kuwajibika na sio chuki.
Mahakama ya kimataifa ilifanya uamuzi kuifaidisha Tanzania wakati fedha
zimeshatolewa na waziri mkuu iliujua huu mchakato. Kamati ni ya PAC na
sio kamati ya upinzani na ina wajumbe 19 kutoka CCM na wajumbe watano
upinzani.
Jambo hili linaivua serikali nguo, na kuvuliwa serikali na kuivua nchi.
Muda umeisha,
Mwenyekiti: Nashukuru mjadala wa amani na anataja ratiba ya kesho pia anaahirisha shughuli za bunge mpaka saa tatu asubuhi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment