BALOZI KAMALA AANZISHA MFUKO WA ZAWADI WA DR. KAMALA "Dr. KAMALA AWARD FUND"
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala
(aliyevaa miwani) akizungumza katika Mahafari ya Kituo cha Chekechea cha
Frorence yaliyofanyika Kigogo Dar es salaam. Watoto mia moja wamehitimu
katika Kituo hicho na wote wamejifunza na kuelewa kusoma na kuandika.
Balozi Kamala amewashukuru Bwana na Bibi Mbezi kwa kuanzisha kituo
hicho. Aidha, Balozi Dr. Kamala ameanzisha mfuko wa zawadi wa Dr. Kamala
"Dr. Kamala Award Fund" utakaokuwa unatoa zawadi kila mwaka kwa mtoto
atakayeonesha kipaji cha uongozi. Baada ya Balozi Kamala kutoa laki moja
za kuanzisha mfuko huo wazazi walimuunga mkono kwa kuchangia laki moja.
Balozi Kamala amehaidi kuchangia milioni moja mfuko huo na riba
itakayopatikana kila mwaka itatumika kutoa zawadi kwa mtoto
atakayeonesha kipaji cha uongozi. Vile vile Balozi Kamala alichangia
shilingi laki mbili na nusu kituo hicho na amehaidi kukitafutia
wafadhili wa kukisaidia.