Bukobawadau

CRDB YAIBUKA KIDEDEA KATIKA TUZO ZA NBAA UPANDE WA MABENKI

 Naibu waziri wa fedha Adam Malima akimkabidhi meneja wa fedha wa benki ya CRDB Sosteness Biseko  tuzo  ya NBAA ya ushindi  katika  uandaaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2013-2014,jumla ya benki tisa zilishiriki ambapo Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la mabenki, hafla hiyo ilifanyika juzi katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
*********

Mashirika binafsi ,taasisi na idara mbalimbali za serikali zimehimizwa   kushiriki katika mashindano ya tuzo zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA katika uandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ili kuboresha hesabu za mashiriki hayo na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara za ndani ya nchi na kimataifa 

Mwenyekiti wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA Profesa Issaya Jairo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa bodi hiyo ulio enda sambamba na utoaji wa tuzo na vyeti kwa washindi  katika uaandaaji  bora wa taarifa za fedha za mwaka ambapo kwa mwaka 2014 jumla ya washiriki 40 walishiriki ambao waligawanywa katika makundi 11 kulingana na huduma wanayo itoa

Katika kundi la mabenki, benki ya crdb ilibuka mshindi  wa kwanza kwa mwaka2013-2014 na kupata tuzo maalumu ya uandaaji  wa taarifa bora  za fedha za mwaka iliyokabidhiwa na naibu waziri wa fehda Adam Malima  kwa meneja wa fedha wa benki hiyo Sosthenes Biseko ambaye akizungumzia ushindi huo amesema ni njia mojawapo ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuendelea kuwa na Imani na benki.
Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya CRDB wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano hayo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau