SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

18 December 2014

DOZI NYINGINE KWA LEO ALHAMISI DEC 18,214

Hata kama kwenu mnajiweza kiuchumi na kifursa kuliko walivyo kwa mume wako au kuliko alivyo yeye, hata kama ulibahatika kwenda darasani kuliko yeye, bado wewe ni mke na haunabudi kumheshimu mume wako kama mume. Nafasi ya juu kijamii, upana wa elimu, uwezo wakifedha au kifursa havitoshi kamwe kufanya utake kuogopwa na mumeo au na wanaokuzunguka, havikufanyi wewe ndio uwe mtoa “orders” na kutaka kila kitu kifanyike unavyotaka wewe. 
Nadhani labda bado hujajua maana halisi ya kuwa “mke”, kama kweli ulimpenda na unamheshimu kama mume na kiongozi wa familia yenu basi vitu na hali zozote za kwako au kwenu hazitaishinda nguvu ya penzi na kwahivyo hautopata shida kumheshimu na kumjali kama MUME, lakini kama kuolewa naye kulilazimishwa na mazingira (kama vile mimba, kujiona unachelewa kuolewa, kushawishiwa n.k) basi lazima dharau itautangulia utu wako.
  Hata kama wazazi wako wanamdharau, na kumpinga mumeo kwasababu walitaka uolewe na mtu wakufanana na hadhi ya familia yenu, bado wewe haunabudi kusimama upande wa mume wako na kuwaonyesha wazazi wako kuwa haukukosea kumfanya yeye chaguo lako. Sasa inakuwaje unasimama upande wa wazazi wako na kumshushia hadhi mumeo? Huyo sio tu baba wa watoto wako, huyo ni mumeo, usijitafutie balaa usizozijua na kuifunga milango mingine ya Baraka na mafanikio kwa tabia hiyo mbaya. Love surpasses everything

1 comment:

Anonymous said...

Yap,nimekupata mtu wangu but ndoa bora ni nyote wawili kueshimiana na kusaidiana kwa kila jambo

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU