Bukobawadau

HAFLA YA KUMPONGEZA MWL-MARTHA BISHANGA YAFANA NDANI YA BUKOBA CO-OP..!!Hafla ya kumpongeza Mwl. Martha Bishanga kwa kustaafu utumishi wa Umma yafana Sana,Hafla hii imefanyika Usiku wa jana Dec 12,katika Ukumbi wa Bukoba Co-Op Hotel.
 Shughuli inaanza kwa furaha ..Wanafamilia wanaingia ukumbini

 Namna hii wakicheza na kuimba wimbo wa 'Nani kama Mama'
Watoto wa Mstaafu mwalimu Martha Bishanga kama wanavyo onekana wakiingia kwa mbwembwe ukumbini na kupata mapokezi ya nguvu kutoka kwa waalikwa.
 Kundi la Walimu linafuata likiongozwa na  Mzee Manyama.
 Sasa anaingia Ukumbini mstaafu Mwalimu Martha Bishanga akiwa amependeza ile mbayaa! Vazi refu alilovaa limemkaa vyema
 Waalikwa ukumbini wakiwa wamesimama wakati Mstaafu akiingia Ukumbini
 Mwalimu Martha Bishanga pichani kushoto na mpambe wake,ambaye ni rafiki yake karibu Mama Matungwa mtaalam wa  Decoration::Advents Deco and Planning kama mtakavyo jionea kumbi umepambwa na kupambika ipasavyo
Mara baada ya mstaafu kuingia ukumbini, Shughuli ikafunguliwa kwa sala takatifu iliyo ongozwa na Bi  Mecktrida Michael Pichani
 EEEE BANA EEEE Muonekano wa Kitu Keki iliyotengenezwa na mtaalam wa fani Mama Simeo!!
 Jamani pale kwenye kutoa sifa mtu na apewe sifa zake BUKOBAWADAU tunachoweza kusema hii ya leo ni  kiboko Kwa Keki..Ni Sheeedah !!
 Bi Georgia Kalikawe na Mama Lugusha pichani ni sehemu ya waalikwa
Meza mbalimbali za waalikwa walio hudhuria hafla hii ndani ya Ukumbi wa Bukoba Co-Op,
 Kushoto ni Mh. Anathory Aman na Mkewe.
  Kutoka katika familia za kichief  ni Bi Anitha Rugalabamu na Mr Devo Rugaibura (Mr & Mrs Divo.
 Kuvaa ni njia mojawapo ya kujiamini kwa mwanamke,Pichani anaonekana Bibie Laty katika 'Smile' Mtoto mkalee, mtoto msomi, ana pozi na muelewa!
 Muonekano wa meza mbalimbali za waalikwa ukumbini.
 Mwalimu Martha Bishanga akitoa Utambulisho.
Watoto wa Mstaafu Mwalimu Martha  Bishanga pichani
Walimu wenzake katika Utambulisho
 Pichani kulia anaonekana Mr. Mkayo
 Kwa vazi hili Credit kwako  Dada Hope Kazimbazi wa Makoko maarufu kama Manywele,tunakupa Credit kwa sababu kuna watu wanashindwa kutofautisha nguo ya kuvaa disco na kwenye party..!!
Katika hili na lile ndivyo mambo yanavyo endelea ukumbini hapo.
 Mr & Mrs Anathor Amani wanapokea zawadi yao ya Keki
 Zawadi kwa Kaka yake ambaye ndiye kiongozi wa Ukoo Dr. Bishanga.
Kwa niaba ya Mme wake Mzee Ngaiza Meneja wa KCU (1990)Zawadi inapokelewa na mwane mkubwa  Ndugu Rweyemamu Victar Ngaiza
 Mdau Samuel Stephen mwenyekiti wa Kamati ya Chakula mara baada ya kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya kamati nzima ya maandalizi ya hafla hii.
 Mwalimu Fabian naye anapokea zawadi ya keki
Shughuli ya kukabidhi zaidi ya Keki 20 kwa ndugu jamaa na marafiki likiendelea kwa kasi.
 Bi Angel, Mrs Nyamoni  baada ya kupokea  zawadi ya keki ya Upendo kutoka mama Mzazi
 Walimu wa Shule ya msingi Kashai,Shule aliyokuwa anafundisha Mwalimu Bishanga hadi kustaafu .
 Mama Adventina matungwa akipokea zawadi yake ya Keki
 Bi Editha  katibu wa kamati ya maandalizi akikabidhiwa zawadi yake ya Keki
 Watoto na wajukuu wa Mwalimu  Martha Bishanga katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya Keki
Sehemu ya Watoto wa kuzaliwa na Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga.
Mama Semeo na Mama Matungwa katika hili na lile wakati Mstaafu akiendelea kukabidhi zawadi ya keki kwa makundi mbalimbali kulingana na umuhimu katika maisha yake ya kazi mpaka kustaafu
Kuhusiana na Keki jamani  mchakato ukiendelea
 Juu ya Keki Hongera Sanamama Simeo,hongera  Dada Angel na kamati yamaandalizi.
 Anaonekana Bibie Editha wa Nicodemus kama kawaida ni mtu tabasamu wakati wote.
Kivutio kingine katika hafla hii ni Wanamama walivyo onyesha umahiri wa kufungua  champagne.
 Wakimpongeza mama yao mzazi
 Bi Anjoy mara baada ya kumpongeza Mama yake Mzazi
 Anaitwa Jamal Kalumuna
 Bi Sharifa wa Athman ShaR wa Badru Mangi Saidi
 Bi Jamila Jamal pichani kulia.
 Pongezi zikiendelea kumiminika
Hakika watu wote wanaonekana wenye furaha katika kumpongeza mstaafu Mwalimu Bishanga.
Katika kuzoom anaonekana Mdau akifanya 'kutweet'
Mwanadada Sarah pichani
 Katika hili na lile ndivyo anavyo onekana mmoja wa waalikwa Ukumbini
Kundi maarufu la Mwanadada Mery likiendelea kutoa burudani safi ya Ngoma za asili.
 Star wa Usiku huu alikuwa  Mr. Kilangani, aliyeweza kutoa historia ya Mstaafu Mwalimu Martha Bishanga kwa njia ya ushairi  yaani sauti iliyo kati ya kuimba na kuongea tena kwa lugha ya asili "Kihaya'
Kibwakizo kikubwa katika ushairi huo kinasema ...'Martha Akanganyira Owomulikubona Omumaisho ganyu, Mwana wa ta Sebastiani Bishanga na ma Paulina Kokunywegeza, Omwabo ni Kiziba Kanyigo Omukyaro kwa Kikukwe...
 'Orugandarwe Mulwanikazi nazira Ente ya Runya,naruga  omumalembo nyarutembo... 'Endelea kuwa nasi mpaka mwisho kwa ushairi kamili hapo badae.
 Mh. Aman mara baada ya kukabidhi zawadi yake ,anampongeza Mstaafu Mwalimu Bishanga
 Mwanadada Hope mara  baada ya kukabidhi zawadi yake kwa mstaafu
Mzee Mshashu akikabidhi zawadi yake
 Walimu wa Shule ya Msingi Kashai wakiwa na zawadi yao
 Bi Angel akiongea kama muweka hazina wa kamati ya maandalizi
Athman na Murshid wakifanya mawasiliano
 Wanafamilia wakishusha bonge laburudani
 Burudani kutoka kwa wanafamilia ikiendelea.
 Sehemu ya Waalikwa wakipata msosi
 Utaratibu wa kupata huduma ya Chakula ukiendelea..
 Ndugu Athmani Bahati akipati mulo safi.
 Taswira mbalimbali mapema kabla ya sherehe ya kumpongeza Mwl-Martha Bishanga kuanza.
 Wakati Bi Husna Khaldi anaingia Ukumbini
 Wakati familia ya Mama Seleda ikiingia Ukumbini
 Mwanzoni wakiingia Ukumbini walimu wa Shule ya Sekondari Kashai
 Upande wa Mapokezi  mambo yalikuwa hivi
 Ni mwendo kwa Kula kunywa na kufurahi
 Bi Shatifa anasema: Safi sana..imekaa vizuri!
 Dada Angel  akiwajibika 
 KUFIKIA HAPA NIKWAMBA:BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
 Picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA  2oo INGIA HAPA>>Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau