Bukobawadau

MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA KAGERA FARMERS CO-OPERATIVE BANK (KFCB) LTD WAFANYIKA DEC 11,2014 MJINI BUKOBA

Mkutano mkuu wa kawaida wa kumi na tano wa Kagera Farmers Co-Operative Bank (KFCB)Ltd uliofanyika tarehe 11/12/2014 katika ukumbi wa Bukoba Co-Op hotel zamani (Yaasila) uliopo ndani ya Manispaa ya Bukoba ,Mgeni rasmi alikuwa Mrajis wa vyama vya ushirika Nchini.
 Pichani ni wajumbe wa Bodi ya (KFCB)yenye jumla ya wajumbe watano wakiwa ni watatu wa kuchaguliwa na wawili wa kuteuliwa.
Wengine walio hudhuria Mkutano huo ni pamoja na Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoani Kagera,wawakilishi kutoka Benki kuu ya Tanzania ,wajumbe wa mkutano mkuu na waalikwa mbalimbali.
 Mwenyekiti wa (KFCB) Gozbart Rugumila akiongoza mkutano huo.
Aidha katika mkutano  aliweza kutengua Bodi ya wajumbe watano imepanguliwa na kufanyika uchaguzi  mpya ulio simamiwa na  Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoani Kagera pichani .,Uchaguzi ambao  wajumbe watatu waliweza kuchaguliwa.
Waliochaguliwa  ni Mwenyekiti Ndugu Gozbart Rugumila naTheonest Rutamingwa kuwa makamu mwenyekiti ,mjumbe wa tatu ni Mr. Pius Mushuga .
 Taswira meza kuu
 Akiongea mbele ya Mgeni Rasmi ,Mwenyekiti wa bodi amesema;''Ninaamini umeishapata maelezo mafupi kuhusu benki yetu na huenda  umebaini kuwa changamoto  kubwa tulionayo ni ufinyu wa mtaji,wenye mali kutotumia benki yao katika shughuli zao za kibenki ikiwa ni pamoja na kufunga akaunti zao na kuhamia benki nyingine''
Swala la Mtaji limekuwa likiongelewa katika kila kikao cha mkutano Mkuu.
Mpaka sasa benki ina jumla ya mtaji wa Tshs.2,011,660,000.Mtaji ambao ni mdogo sana kulingana na changamoto za biashara ya kibenki yenye ushindani mkubwa.
Mwenyekiti anaendelea kusema kuwa;..Swala la wanahisa kuongeza hisa licha ya kuwa la lazima kwa mujibu wa sheria,ni muhimu pia kwa biashara ya benki kwani uwezo wa benki kufanya biasha ambapo biashara kuu ni kukopesha kunahitaji mtaji mkubwa.
Kulingana na changamoto kadha wa kadha ,benki imeshindwwa kupata faida kwa ama matumizi ya kudumu au yasiyobadilika kuwa makubwa tofauti na kipato kinachopatikana,Matumizi hayo hasa ni mishahara ya wafanyakazi na maslahi yao mengine. 
Kwa kuzingatia hali hio benki imeamua kupunguza matumizi ya uendeshaji ikiwami pamoja na wafanyakazi na utaratibu unaendelea.
'Benki inaamini wafanyakazi watakaobaki watafanya kazi kwa ufanisi na kuifanya benki itengeneze faida'pichani anaonekana Mr. Maluma afisa mikopo (KFCB)
Mjumbe  akijaribu kutoa ushauri kutokana na maelezo yaliyo tolewa juu  kudorora kwa uchumi duniani mwaka 2008 na kupelekea benki ya KFCB kuto kutengamaa kama ilivyo kusudia.
 Kaimu meneja mkuu wa Benki ya KFCB akitolea jambo ufafanuzi
Mjumbe akiuliza swali 
 Meneja wa (KFCB) akifafanua hali ya changamoto zilizopo kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya ushirika na ujasiriamali na elimu ya kuheshimu mikataba ya mikopo kwa wateja  sambamba na juhudi mbalimbali zilizofanyika katika kukusanya madeni mbalimbali
 Sehemu ya wanahabari
 Mmoja wa Staff Benki ya wakulima ya mkoa wa Kagera (KFCB Ltd).
 Mwakilishi kutoka benki kuu ya Tanzania (BOT) akitolea jambo ufafanuzi
 Kushoto ni Bw Frank Muganyizi mwenyekiti mpya wa KCU (1990)Ltd ,anaye fuata ni Meneja Mkuu wa KCU (1990)Ltd  Ndugu Vedasto Ngaiza
Ni mkutano mkuu wa kawaida wa kumi na tano wa Kagera Farmers Co-0perative Bank (KFCB)
 Wajumbe wa mkutano mkuu kutoka  maeneo mbalimbali wakiendelea kuuliza maswali.
 Kwa umakini mkubwa wajumbe wakipitia  makaburasha
Benki pia ina mkataba na mfuko wa pembejeo wa kukopesha fedha kwa ajili ya pembejeo za kilimo.
Mjumbe akichangia swala la Umuhimu wa Saccos
 Mzee wa kazi Mc Lutakwa kama anavyo onekana pichani.
Muonekano wa wajumbe mkutano ukiendelea.
 Wakati mchakato wa kura unaendelea
Camera etu ikicheck na wadau walio hudhuria mkutano huu.
Muonekano wa Wajumbe wakati mkutano ukiendelea.
 Mwakilishi wa NSSF.
Mwakilishi kutoka ofisi  ya Mrajisi wa vyama vya ushirika Nchini
 Ndugu Rugumira ambaye ndiye mwenekiti wakati akiomba tena nafasi hiyo
Mjumbe mpya katika bodi ya KFCB  Ndugu Pius Mushuga pichani kulia wakati akijinadi
 Mwisho Mwenyekiti na wajumbe wa bodi wanatoa shukrani za dhati kwa Idara ya maendeleo ya Ushirika kwa ushirikiano mkubwa walionao ikiwa ni pamoja na Uongozi wa 'UNION' KCU (1990)Ltd  na mfuko wa udhamini wa mazao (KFTF)
Bango la Bukoba Co-Op hotel
 Sehemu ya Maegesho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau