HII KWA LEO KRISMAS:We need to see the difference
Waraka wa kwanza wa Yohana 3:18 "............ tusipende kwa neno, wala
kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli". Hivi mpaka lini wewe utaendelea
kusema tu kwa maneno "I love you" "na kumiss sana" "u mean a lot to me" "
siwezi bila wewe" wakati hakuna hata tendo moja linalo support hayo
maneno yako? Kujali hujali, msamaha hujui kuomba, shukrani huijui
kabisa, kila siku unasema utajirekebisha lakini hata dalili za
kurekebishika hazionekani, kila kukicha unarudia makosa yale yale ya kila
siku, kama kweli unampenda mbona unashindwa kubadili hizo tabia
asizozipenda ili kumruhusu akupende zaidi??. Unakuwa mzigo badala ya
kuwa wa msaada kwa mpenzi wako, nakubali kabisa kwamba kusema
"nakupenda" nitajirekebisha" ni maneno ya kutia moyo lakini pale
yanapozidi kusemwa pasipo vidhibiti yanapoteza ladha na nguvu yake. Acha
kuuza chai kwa maneno yako matupu yasiyoweza kuvunja mfupa, mpenzi wako
hataki maneno matupu, anatamani kuona matendo kutoka kwako, maneno
matupu hayashibishi kiu ya penzi bali maneno yenye viambatanisho vya
matendo. Kama ni maneno tu hata kasuku anayo, we need to see the
difference - Chris Mauki