Bukobawadau

HAFLA YA LUGOYE DAY ILIYOFANYIKA KIJIJINI KYELIMA ISHUNJU DEC 28, 2014

Prof.Joseph Kahamba pichani ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kikundi kinachojumuisha wanaume 20 kutoka katika Kata za Ishozi, Gera na Nshunju kijulikanacho kama  'Lugoye Social Club'akiongea katika hafla ya mwisho wa Mwaka iliyofanyika Kijijini Kyelima Ishunju kwa Ndugu Kamugisha.
Mr Bitus L. Nyema na Mr Kamugisha ambaye ndiye mwenyeji wa shuhuli hii siku ya leo
 Mwenyekiti wa Lugoye Prof.Joseph Kahamba akiongelea  mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na historia ya Umoja huo sambamba na malengo mahususi ikiwa ni pamoja na kukumbuka Nyumbani na kushiriki kuchangia maendeleo.
Kwa siku ya leo Lugoye kama jamii inayoweza kushirikiana katika maswala mengi yanayo husu jamii ,hukutana kila mwisho wa mwezi na kuona namna wanavyo weza kuchangia jitihada za Serikali katika kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.
 Omwana  Florida Lutinwa akifutiwa nawadau wengine
Wakiendelea kupata chakula.
 Prof.Godeliver Kagashe Kahamba  makamu mwenyekiti wa wanawake wa Lugoye akisoma maendeleo ya Umoja na ikiwa leo hii Dec 28,2014 wamefanikisha kuchangia Ujenzi wa Kisima cha maji kijijini hapa hii mwaka 2011 waliweza kutoa msaada katika Dispensari ya kyelima iliyopo  kata ya Ishinju sehemu tuliyopo leo,mwaka 2012 vitabu na vifaa vingine shule ya Msingi Gera.
Sehemu  ya Kikundi cha wanawake wa Lugoye walioolewa Ishozi, Gera na Nshunju wanaoishi  Jijini Dar es Salaam wakieongea mbele ya wananchi walio hudhuria hafla hiyo .
Akina mama hawa walianza kwa kusaidia makundi ya watu mbalimbali wenye matatizo kama vile waathirika wa Ukimwi,watoto yatima,wanane n.k hasa walioko mkoani Dar es salaam.
 Lakini tangu mwaka 2010 waliona wasaidie wahitaji waliopo nyumbani na walianza kwa kutoa msaada katika shule ya sekondari ya Lugoye iliyoko kata ya Ishozi na mwaka 2011 waliweza kutoa msaada katika Dispensari ya kyelima iliyoko kata ya Ishinju na mwaka 2012 vitabu na vifaa vingine shule ya Msingi Gera.
 Mr Mtagwaba pichani, ndugu wa familia ya Kamugisha
 Mzee Yusutas Kamugisha akitoa neno kwa niaba ya familia ambapo alitumia fursa hii kuwashukuru watoto wake kwa kufuata Nyayo zake katika harakati za maendeleo.
 Wazee wafamili 'Abanyaluganda wakimsikiliza kwa makini Mzee Yustas Mugisha
Mchakato wa Vyombo vya habari , na matukio mengine kwa ajili ya kumbukumbu 'Lugoye Day'.
 Mr Charles Kamugisha katika picha na baba yake mzazi ,Mzee Yustas Kamugisha ,diwani miaka 20 iliyopita, ni mzee mpambanaji historia inaonyesha ndiye aliyekuwammiliki wa mabasi ya Kumekucha na Lugoye.
 Meza kuu kutoka kushoto ni aliyekuwa Mwenyekiti  wa Lugoye mwaka uliopita Mzee Erasto Machume, Mh. Diwani kata Ishunju na Mwenyekiti Prof.Joseph Kahamba
Ndugu Respikius akitoa shukrani kwa Wanalugoye kwa niaba ya Vijana wote wa maeneo husika
 Watoto wa familia ya Mzee Erasto Machume.
Ikiwa ni jumla ya akina mama 20 ingawaje hapa wapo wachache kutokana na baadhi ya wenzao kuwa na majukumu mbalimbali,nia na majukumu yao ni kusaidiana katika shida na raha pamoja na kusaidia jamii katika kutatua matatizo mbalimbali yanayo wakumba.
Wananchi wakiwa tayari kwa ajili ya kusikia harakati za maendeleo za Wanalugoye
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Lugoye Social Club  Prof. Joseph Kahamba,akifuatiwa na Ndg Josiah M. Munaz  na Nd Bitus L. Nyema.
 Sehemu ya waalikwa na wanachama wa Lugoye Social Club wakifuatilia Burudani.
Wawindaji wakitoa burudani kwa umahiri mkubwa.
Kundi la hili la Wawindaji wa Kijiji cha Kyelima wamekuwa wakitoa burudani katika sehemu mbalimbali
Sehemu ya Wageni waalikwa
Masudi na Msafiri wakifuatili kinacho endelea.
Wawindaji wakionyesha Ngozi ya mnyama pori mkali ambaye alikuwa anasumbua Kijiji.
Mr. Bitus L. Nyama mwanachama wa Lugoye anatoa mchango wa shilingi laki tano kwa Wawindaji.
Taswira mbalimbali Ukumbini
Wawindaji wakisoma Risala yao mbele ya meza kuu.
 Muonekano wa mavazi ya Wawindaji hao wakati wakisoma Risala
 Wawindaji wa Kienyeji wakikabidhi zawadi yao kwa mwenyekiti wa Rugoye Prof. Joseph Kahamba
 Katikati  anaonekana Mlangira Ben Kataruga mara baada ya kukabidhiwa zawadi na wawindaji kama Mwanachama wa Lugoye anayetoka eneo la Gera,
 Ndg Wenseslaus Rwiza pichani kushoto akifurahia jambo na wanachama wenzake , katikati ni Mwenyekiti wa Lugoye Prof.Joseph Kahamba na Mlangira Ben Kataruga
 Prof. Godeliver K. Kahamba na  na Bi Specioza Machume pichani.
Wakibadilishana mawazo wakai sherehe inaendelea
 'Abajunansi'katika picha ya kumbukumbu na Mlangira Ben Kataruga na Ndg Charles Kamugisha.
Sehemu ya wazee waliojitokeza katika hafla hii ya mwisho wa mwaka iliyo andaliwa na mmoja wa Wanachama wa Luguye Ndugu  Charles Kamugisha.
 Mr. Wencheslaus  Rwiza na Mr Ben Mulokozi wanachama Lugoye Social Club.
Mwenyekiti Prof.Joseph Kahamba katika picha na Mzee Josian L. Munazi
Omwana Florida Lutinwa.
 Ndugu Msafiri pichani akiongoza harambee ya kuchangia miradi mbalimbali.
 Wawindaji wa kienyeji wanaokabiana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na leseni
Mlangira Focas  Lutinwa akitoa mchango wake kwa ajili ya Kikundi cha wawindaji.
Ndugu Masudi  akikabidhi mchango wake ,huyu Masudi yeye sio mwanachama wa Lugoye bali ni Bodyguard wa Ben Mulokozi kazi yake ni kumlinda kutokana na hatari yoyote kama wizi, utekaji, mashambulizi, vitisho au kero za hapa na pale.
 Adoroph John kiongozi wa wawindaji akitoa shukrani kwa Wanalugo na wananchi waliochangia  fedha  kwa ajili ya kununua mahitaji yao mbali mbali kama sare na vitendea kazi.
 Kiongozi wa 'Abajunansi" akitabasamu  kufikia malengo baada ya kuchangiwa na Wanalugoye kiasi cha shillingi milioni mbili. [2,000,000]
  Kwa hamasa kubwa  kutokana na fedha walizo zipata,kiongozi huyo wa kundi la wawindaji maarufu kam  'Abajunansi" anatoa kiasi cha shillingi laki moja kama mchango kwenyeujenzi  wa kituo cha  afya unao endelea kijijini Kyelima Ishunju.
 Fedha hizo zinakabidhiwa kwa Mh. Diwani wa Kata  ya Ishunju
Wanalugoye wanamchangia Fedha  Kijana mlemavu kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba yake
Baada ya adha ya kuishi ambapo  nyumba yake ilisombwa na maji
Mr Deo na Mr Ben.
Mlangira Ben Kataruga kwa mara  nyingine katika harakati za maendelea kupitia kufia ya Lugoye  anachangia kiasi cha shillingi laki mbili kwa ajili ya ya Ujenzi wa Chumba cha Darasa .
Mr. Ben Mulokozi akiwaaga wageni
 Mc Baraka katika picha na mwenyeji wa  eneo hili Bro Kamugisha
Mwenyekiti wa Kijiji akitoa shukrani zake za dhati kwa Mlangira Ben Kataruga
PITIA SEHEMU NDOGO YA VIDEO YALIYOJIRI LUGOYE DAY DEC 28,2014
ENDELEA KUWA NASI KWA MATUKIO KAMILI YA VIDEO.
Next Post Previous Post
Bukobawadau