SEARCH -TAFUTA

.

SIR.LOOM INC

24 December 2014

HAYA NI MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI ....!

Jina Tibaijuka tafsri yake katika kiswahili sanifu ni "huwahawakumbuki" yaani watu huwa hawakumbuki walikotoka au hawakumbuki watu waliowafikisha hapo walipo au huwa hawakumbuki wale waliowafanyia mema au huwa ni wepesi wa kusahau mambo muhimu yumkini yaliyowawezesha kufika hapo walipo.
Swali la kujiuliza ni hili je, Prof Tibaijuka ilikumbuka hali ya watu wake aaliomuweka madarakani? Je alikumbuka heshima aliyokuwa ameijenga kwa muda mrefu kimataifa? Je alikumbuka aina ya nchi ambamo yeye ni kiongozi wake?
Ni kutokukumbuka kwake yamemkuta yaliyomkuta. Je siku ile anaitisha mkutano wa waandishi hakukumbuka kuwa Rais atafanya maamzi? 
Je hakukumbuka kaamba alitakiwa asubiri mkubwa aseme? Oh, kutokukumbuka!
Wahaya huwa tunamsemo usemao "eibara lita nyinalyo" yaani jina humuua mwenyewe. Wazazi tunahitaji kujua na kutafakari sana majina tunayowaita watoto wetu our names can determine or contribute to o ur destine wapendwa?
Ukifanya mnyambulisho wa nomino Muhongo waweza pata vitu ukiondoa mu unabakina hongo yaani rushwa, ukiondoa h unabakiza muongo yaani mtu asiyesema ukweli, pia ukiondoa n unapata muhogo yaani cassava chakula dhalili na cha msimu kwa kabila fulani.
Na hayo yalikuwa mazungumzo baada ya habari

1 comment:

Anonymous said...

Tibaijuka, ni ubini wa mumewe. Lakini la kuvunda halina ubani, yatasemwa mengi!

 

WASILIANA NASI KUPITIA 0715505043 / 0784505045 0768397241 / 0754505043

.

SIR.LOOM INC & MC BARAKA

.

IDADI YA WATU