Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Bw Nape Nnauye ameyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wakati umefika utaratibu wa kuunda tume kila jambo ufe kwani ni matumizi mabaya ya fedha na mwisho wa siku zinaleta ripoti machungungu ya jambo yakiwa yameisha hivyo haifanyiwi kazi tena huku akielezea namna CCM ilivyofanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha kwa mara ya kwanza Bw Nape amevipongeza vyama vya upinzani kwa
hatua vilivyofikia lakini akadai kuwa kwa umri waliofikia tangu
vianzishwe hapa nchini havikupaswa kuwa hatua vilivyopo hivi sasa bali
walitakiwa kuwa mbele zaidi huku akivitaka kutekeleza yale yote
waliyoahidi kwa wananchi waliowapa dhamana na kuongeza kuwa furaha ya
CCM ni kuona mfumo wa ushindi unakuwa.
0 comment:
Post a Comment