LIPUMBA:Walioshindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wawajibishwe.
Chama cha wananchi -CUF- kimemtaka
rais Jakaya Kikwete kumuwajibisha waziri mkuu na waziri wa tamisemi kwa
kushindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa na baada ya kuibuka
dosari kubwa zikiwemo kukosekana kwa wino, majina ya wananchi na
karatasi za kupigia kura jambo lililote vurugu na kusababisha vituo
vingi kurudiwa uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa CUF taifa Prof.
Ibrahim Lipumba ametaka serikali kutekeleza makubaliano ya vyama vya
siasa na tamisemi yaliyotaka uchaguzi tume ya taifa ya uchaguzi ndio iwe
na dhamana ya kusimamia uchaguzi, pamoja na daftari la wapiga kura
litumike katika uchaguzi wa serikali za mita pamoja na kuingizwa kwa
kipengeke cha maadili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha kutokana na vurugu zilizojitokeza katika uchaguzi wa serikali
za mitaa katika baadhi ya maeneo, Profesa Lipumba amelitahadharisha
jeshi la polisi kuhacha kutumia nguvu kwa ajili ya kulinda maslahi ya
baadhi ya vyama ili kuepusha vurugu zisizoza lazima katika uchaguzi mkuu
unaotarajia kufanyika mwakani.