Bukobawadau

MTOTO AOKOLEWA NDANI YA SHIMO LA CHOO

Mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja ameokolewa na wasamaria wema toka kwenye shimo la choo akiwa bado  hai bada ya mama yake mzazi kumeza dawa kwa lengo la kutoa mimba na kumtupa ndani ya shimo hilo.
ITV imefika katika kituo ch afya cha PK  kilichopo kibaoni tegeta manisipaa ya kinondoni  jiji la Dar-es-salaam na kukutana na harakati za wahudumu wa afya wakijaribu kunasua mabaki ya kinyesi kwenye mwili wa kiumbe huo,aliyetupwa kwenye shimo la choo katika eneo la tegeta machakani.
Wakiongea na ITV baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mama aliyekuw ana muhifadhi kwa muda binti anayedaiwa kutupa kichanga hicho wamesema kuwa watoto walipata taarifa ya mlio wa sauti wa mtoto ukisikika toka kwenye choo cha shimo kabla ya kuchukua hatua za kuvunja choo hicho na kutoa mwili wa kiumbe huyo.
Bi Aisha Mohamedi anayedaiwa kutupa kichanga hicho kwenye shimo la choo amesema kuwa,awali mzazi mwenzake alimlazimisha kutoa mimba hiyo bila mafanikio na hata kudiriki kumtishia kwa silaha aina ya kisu,na ndipo alipozidiwa na kupewa vidonge na mzazi mwenzake kwa minajili ya kutoa ujauzito huo na kukiri kujutia kosa lake hilo.
Mganga mfawidhi katika kituo cha afya cha PK Dkt Mashaka Mwanula amethibitisha  kupokea mtoto huyo wa kiume aliyeokolewa baada ya kutupwa ndani ya choo na hivyo kumpatia huduma ya kwanza kwa kumsafisha huku wakitarajia kumpeleka katika hosip[itali ya wilya ya kinondoni mwananyamala kwa uchunguzi zaidi wa afya ya mtoto huyo,juhudi za kumpata kamnada wa polisi mkoa wa kipolisi kinondoni ACP Camilius Wambura kuthibitisha tukio hilo zinaendelea.
Next Post Previous Post
Bukobawadau