BALOZI KAMALA AKARIBISHWA JIJINI WETTEREN UBELIGIJI
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akilisikiliza
maelezo kuhusu zawadi aliyokabidhiwa kama ishara ya kumkaribisha jijini
Wetteren Ubeligiji. Anayetoa maelezo ni Mhe. Live De Gelder Mkuu wa
Idara ya Ustawi wa Jamii jijini Wetteren. Balozi Kamala leo atatembelea
viwanda mbalimbali jijini Wetteren na atakutana na Wafanyabiashara
kueleza fursa za biashara na uwekezaji Tanzania.