Bukobawadau

MSIBA WA BI LETICIA MATTEI RWECHUNGURA

Tunasikitika kutangaza kifo cha ghafla cha  dada yetu mpendwa Leticia Mattei Rwechungura kilichotokea hapa Ujerumani tarehe 06.01.2015. Mazishi yatafanyika hapa Ujerumani Königswinter, karibu na mji wa Bonn tarehe 24.01.2015. Misa itaanza saa tano asubuhi (11:00 a.m.), katika Kanisa la St. Michael Niederdollendorf, Petersbergerstr. 14, 53639 Königswinter.
Dada Leticia Mattei alikuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko South Sudan (UNMIS) - United Nations Mission in Südan, Eastern Equatoria State of Torit-Sudan. Aliugua muda mfupi na kufariki dunia katika hospitali iliyoko mjini Bonn hapa Ujerumani. Watanzania wote walioko hapa Ujerumani, nyumbani Tanzania na ulimwenguni kote wameshtushwa na kifo hiki cha ghafla cha kuondokewa na mama yetu na dada yetu mpenzi Leticia Mattei. Tutamkumbuka daima kwa kazi kubwa alizoifanyia nchi yetu ya Tanzania, bara la Afrika na dunia nzima kwa ujumla.
 Kwa yeyote atakayependa kutoa sanda yake, tunaomba michango itumwe moja kwa moja kwa mtoto wa marehemu:
Diana Kajuna
IBAN: DE76 3806 0186 5501 3030 13
BIC: GENODEDIBRS
Kreditinstitut: Volksbank Bonn Rhein-Sieg eG.
 Tunaomba sana ili tuweze kutekeleza mipango hii vizuri ya kumsindikiza dada yetu kwa heshima zote, wale wanaopenda kuhudhuria mazishi haya wawasiliane na mratibu wa shughuli hizi Nd. Majura, ili tupate orodha kamili ya wale wanaokuja ili itusaidie kuandaa mambo mengi ya muhimu. Kwa wale watakaopenda kupata malazi (ya hoteli), kadhalika tunaomba wawasiliane na Dr. Isack Majura kuanzia sasa kupitia:
Tel. +49 173 7089513
e-Mail: IMajura@aol.com
Germany.
 Pichani ni ndugu wa familia ya Marehemu Leticia Mattei Rwechungura wakiwa msibani Nyumbani  kwao jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba huo jijini Dar es Salaam ,siku moja moja kabla ya wanafamilia kusafiri  kuelekea nchini Ujerumani Königswinter,kwa ajili ya kushiriki mazishi
 Wanafamilia kama walivyokutwa na Camera yetu msibani hapo.
BUKOBAWADAU BLOG tunatoa pole kwa wanafamilia kufuatia kifo cha ghafla cha dada yetu mpendwa Bi Leticia Mattei Rwechungura.
 Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen!
Next Post Previous Post
Bukobawadau