Bukobawadau

SKYLIGHT BAND WAZIDI KULITIKISA JIJI LA DAR WASAJILI VIFAA VIPYA AKIWEMO JOHN MUSIC

Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Kifaa kipya ndani ya Skylight Band John Music akiimba kwa hisia kaliii huku akipewa sapoti na Wenzake wa kwanza kushoto ni Baby na wa pili kutoka kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na kulia ni Jessie
Wanaume wa shoka wa Skylight Band kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakionyesha mbwembwe zao za kulisakata sebene kwa mashabiki wao, ambapo jioni ya leo watakuwepo kama kawaida kwenye kiota cha maraha Thai Village
Jessie(katikati) akiimba kwa raha zakee ndani ya Thai Village akipewa sapoti na Baby pamoja na Aneth Kushaba AK47
John Music akiiendelea kutoa burudani ya nguvu huku akipewa sapoti na Wenzake wa kwanza kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na wa pili kutoka kushoto ni Baby na kulia ni Jessie
Sam Mapenzi akiimba Naija Flava njoo leo umshuhudie kwa macho yako...Skylight Band ndio kila kitu huna haja ya kwenda disco unapata kila kitu hapa hapa.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa Meneja wa Band Aneth Kushaba AK47, Sam Mapenzi na Sony Masamba kwa pamoja wakiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) kwenye kiota cha maraha cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita ambapo leo wataendelea kutoa kuwaburudisha mashabiki wake kama kawaida kuanzia saa tatu usiku.
DSC_0021
Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na muziki safi kabisa wa ladha na vionjo vya kila aina ikiwemo Reggae, Kwaito, Naija Flava, R&B, Zouk na zingine kibao bila kusahau sebene pale kati Joniko Flower anahusika sana sambamba na Sony Masamba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau