Hali ya sintofahamu ilianzia katika ofisi CUF Temeke pale mwenyekii wao Profesa Lipumba alipowatangazia wafuasi hao kuwa hakutakuwepo na maandamano ya kuelekea katika viwanja wa Zakhem na badala yake atakwenda mwenyewe katika mkutano huo kuwatangazia wananchi ambao tayari walikuwa wameanza kukusanyika huko katika eneo la mkutano.
Baada ya tangazo hilo safari ikaanza na ndipo mvutano ukaanza baina ya polisi na viongozi wa CUF.
Baada ya mabishano na majadilino ya muda mrefusafari ikaanza tena kutokea Temeke kuelekea Zakhem.
Msafara huo ulipofika mtoni kwa azizi likatolewa agizo lingine la kusitishwa kwa msafara huo
Baada ya majadiliano hayo hali ya hewa ikabadilika temeke ikageuka kuwa iraq ndogo.
Baadhia ya mabomu yaliyokuwa yanarushwa yalidondoka katika makazi
ya watu likiwemo darasa dogo la wanafunzi wenye umri usozidi miaka
mitano ambapo walionekana wakitokwa machozi na makamasi huku mwalimu wao
Bi Halima Semsela akidaia kuna watoto wengine hajui walipokimbilia
0 comment:
Post a Comment