BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA
Balozi wa China nchini Tanzania LU Youqing amewasili mkoani
Kagera leo alasili tarehe 27/01/2015 kwa ziara ya siku
mbili kukagua eneo lililotengwa na
serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa
kilichohaidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo
mwaka jana Oktoba 2014.
Balozi LU akionyeshwa eneo litakapojengwa chuo
Akimkaribisha mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa John Mongella
alimweleza Balozi LU kuwa mkoa wa Kagera una fursa nyingi za uwekezaji ambazo
ni pamoja na uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo vya kusindika bidhaa
mbalimbali ili kuinua uchumi wananchi na mkoa kwa ujumla.
Bw. Mongella alimwomba Balozi LU kufikiria kuleta wataalamu
wa afya hasa madaktari kutoka nchini mwake hususani katika haospitali ya Rufaa
ya mkoa ili kutoa huduma kwani mkoa upo mbali sana na hospitali za Rufaa za
taifa jambo ambalo huleta usumbufu kwa wagojwa wanaohitaji huduma za hospitali
za rufaa.
Balozi LU katika kutoa salaamu zake alisema kuwa amefurahi kufika mkoani Kagera kwa mara ya
pili na akasifu mkoa kwa kuwa na hali nzuri ya hewa na kubarikiwa katika nyanja
mbalimbali za kiuchumi. Aidha, alisema kutokana na urafiki wa nchi mbili za
Tanzania na China amefurahi kuwa sasa kutakuwa na alama ya urafiki huo katika
mkoa wa Kagera.
Pamoja na kuusifia Mkoa wa Kagera imeisifia serikali ya
Tanzania kwa kutekeleza miradi ya maendeleo akisema kuwa ukipita mikoani unaona mabadiliko makubwa
kuliko ilivyokuwa hapo nyuma. Ambapo
alisema kuwa serikali ya China imewekeza na kutekeleza miradi ya maendeleo
nchini Tanzania yenye thamani ya bilioni 3.15
dolla za kimarekani kwa
mwaka 2013/2014.
Balozi LU alitembelea kiwanja cha hekta 26,000 kilichopo
eneo la Kahororo katika Halamashauri ya Manispaa ya Bukoba ambapo chuo cha
ufundi (VETA) kitajengwa na kujionea mwenyewa kitakapojengwa chuo hicho. Pia
alitembelea shule ya Mgeza Mseto ambako aliwahi kutembelea na kutoa msaada wa
komputa ili kuona wanafunzi wa shule hiyo maendeleo yao.
Katika shule ya msingi Mgeza Mseto yenye wanafunzi wa bweni
na kutwa pia inapokea watoto wa aina tatu, watoto wenye albinisimu, watoto
wenye ulemavu wa viungo, na watoto wa kawaida,
Balozi LU alisema amefurahi kuwaona tena na kuhaidi kutoa msaada zaidi
wa komputa ili watoto waweze kila mmoja kujifunza komputa.
Katika maelezo yake Balozi LU aliufananisha mkoa wa Kagera
na Jimbo la Chandog la nchini China na kusema kuwa atahakikisha unaungaisha
urafiki kati ya mkoa wa Kagera na jimbo hilo ili kuleta maendeleo zaidi Kagera.
Vilevile alisema atahakikisha anfanya mpango wa Tanzania hasa mkoa wa Kagera
unakuwa na utaratibu wa kubadilishana walimu kutoka nchini China.
Maeneo ya uwekezaji ambayo mkoa umeyatenga kwa ajili ya
uwekezaji ni pamoja na Kilimo cha kisasa katika maeneo mbalimbali, Ufugaji wa kisasa
wa samaki, Ujenzi wa bandari ya Kemondo(contena terminal) na ufugaji wa kisasa wa nyuki pamoja na
ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA)
Balozi LU akicheza nngoma uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili
Balozi LU akisaini kitabu cha wageni Bukoba airport
Balozi LU akipokea zawadi toka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto
Balozi LU akipokea zawadi toka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto
Katika picha ya pamoja.