Bukobawadau

VALENTINE DAY ILIVYONOGA NDANI YA LINAS

Ikiwa Valentine day ndio imeisha juzi kati ,nasi Bukobawadau  kama kawaida tunakufikishia kile kilichojiri kwa Usiku wa Valentine ndani ya Ukumbi wa Linas Night Club,Jumba la Starehe lenye kila sifa  maarufu kama 'Kisima cha burudani'
 Kwanza kabisa  tutumie fursa hii kuwapongeza kwa dhati kabisa waandaaji wa Shangwe hizi maarufu kama 'Valentine  Lovers' Dinner and Talk' nao si wengine ni  Zachwa Investment kwa ushirikiano mkubwa na  Shemeji Investment
 Hakika jamaa walionyesha kitu tofauti kabisa ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba it was fabulous!
 Mambo yalikuwa bam bam ,mwanzo mwisho kwa mpangilio mzuri  kabisa,bila kumungunya maneno ni kwamba wale waliohudhuria watakubaliana nasi kwamba walipata burudani zenye ubora wa aina yake.
  Sasa ni muda wa ngama kama inavyo onekana pichani,hapa kuna chakula cha kila aina na kitamu!
 Chakula kilikuwa kimeandaliwa vizuri Wadau walichagua menu mfano wa bandle za kuongelea kwenye mtandao, wapo waliobeba firigisi full wengine ndizi utumbo, wengine Vyapati vyapati, sambusa ,Wali na tambi  binafsi nilibeba 'Nkoko mix Pilau masala na salad kidogo'
Bukoba mambo yalipendeza kwa kweli
  
Kila mtu namna ajuavyo katika kuthibitisha upendo wake kwa mwenzake,kwakweli Linas ilipendeza sana!
Dyner Van Jimmy na Azza B  ni mashahidi katika hili
 Wakati Msanii Barnaba Boy' kutoka katika jumba la vipaji la THT, akifanya yake ndani ya Ukumbi waLinas Night Club
 Moto wa burudani ukiendelea kulindima huku ukikolezwa kwa mbali na vionjo vya mduara NA Muimbaji na mtunzi Amini Mwinyimkuu 'Amini' mwenye kipaji cha kipekee kabisa
 Mh. Ibrahim Maburuki akifurahia kinacho ukumbini
Katika picha kushoto ni Mdau Sajidu  na Mr & Mrs Avit.
Taswira mbalimbali  Ukumbini
 Mwanzo wa Bukobawadau kukupa furaha  , tuwe wote mpaka mwishoni
 Mwanadada Faidha pichani kulia akizungusha jicho wallah ni 'Changamoto'
Mratibu wa Shughuli hii Ms Gyna Zachwa kama anavyo onekana pichani akiwajibika
Furaha ,matukio na shangwe za Usiku wa Valentine  zenye ubunifu wa kutosha!
Mr & Mrs Nyamoni katika kushow love
 Katika ku show love mtu na wake pichani ni Mr & Mrs Avith

BUKOBA katika Usiku wa siku inayolenga kuimarisha upendo kati yako na mtu mwingine yeyote
 Matukio ya Valentines  kupitia BUKOBAWADAU tukiwa ndani ya Linas Night Club kila mtu na ampendae akisherekea sawa na wapenzi wengine wote kte Ulimwenguni
 Blonzo Da Öñè na mpenzi wake wakilishana Keki iliyo andaliwa maalum kwa ajili ya wapendanao
 Meza ya Mdau Sirinyo Gozibert na OMG Sajidu
 Familia ya Mzee Mganyizi hawa ni sehemu ya waandaji kupitia kampuni yao Zachwa Investment
Mr Bube na Mr Deo Lugaibura (Mlangira )
 Mr.Bube akikabidhi zawadi kwa mume na mke waliopendeza kwa usiku huu (best couples)
 Katika picha ya pamoja na Mme na mke waliopendeza
 Mtu mmoja mmoja waliopendeza Ukumbini
 Zawadi kwa Kijana maarufu aliye onekana kupendeza zaidi kwa usiku huu
 Mr Zuri Mkurugenzi wa mghahawa maarufu mjini hapa uitwao ROSE CAFE
Hii ni moja katika ya picha kwakweli!
Binti Zachwa mbele ya Camera ya Mwanalibeneke wa Bukobawadau
 Kushoto ni Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani
 Taswira ukumbini watu wakishangazwa jinsi mambo yalivyonoga

 Mambo yanavyo vutia watu wakishangazwa na mng'ao ukumbini na kufurahia show inayoendelea
 Barnaba Boy akifanya yake
 Ukumbi wa Linas ukivutia zaidi
 Show kali ikiendelea ni Kadansee ya hatari


Kwa taarifa zaidi kumbuka ku'like ukurasa wetu wa Facebook kupitia hapa>>Bukobawadau Entertainment Media
 Tazama namna watu walivyopendeza ukumbini
 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Amin Mwinyimkuu 'Amin' na Barnaba Boy wakipagawisha kisawasawa.
Pamoja na mambo mengine yote yaliyo endelea  mwisho wa siku wadau wakahitai uwe na kumbukumbu bora ya siku hiyo,hapo ndipo Bukobawadau na timu nzima ya Nyumbani Studio tulipo onyesha utofauti .
Wadau wakiwa eneo la Nyumbani studio wale wataalam wenye uwezo na kipaji cha kupiga picha na kumfanya mtu anukie kiujana ata kama age imeenda
 Tukio watu maarufu wakipata Ukodak kabla ya shughuli kuanza kwenye Red carpet
 Bibie Anitha akicheck na Camera yetu
 Mrembo akipata picha kwenye Red Carpet
Anaitwa Mc Jerry Mkurugenzi wa Shemeji Investment
Mdau Fide Blonzo Da Öñè katika Ukodak

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu habari na matukio mbalimbali tunayokuwa nayo  tunakukumbusha Ku'Like' ukurasa wetu kupitia link  hii hapa>>Bukobawadau Entertainment Media
Unaambiwa NyumbaniStudio‬ ni chaguo sahihi kwa muonekano wa kistaa
  Ingawa sina utashi na hakika kuyasema mengine... ila ni mchangamfu pia mzuri wa sura na umbo!
Mpambanaji kutoka Nyumbani Studio akiwa amekula pouziiiiii
Mwanadada akiwa amejipanga vyema usiku wa Valentine ndani ya Linas Night Club

 Mr & Mrs Avith katika pozi moja matata.
Mwisho  BUKOBAWADAU BOG tunatumia fursa hii kukujuza kuwa tunazo  nafasi za matangazo katika mtandao wetu kwa bei nafuu,Pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Next Post Previous Post
Bukobawadau