Bukobawadau

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KASHAI HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MILIPUKO

Wanafunzi wa shule ya msingi Kashai iliyopo mjini bukoba wapo hatarini kukumbwa na maradhi mbalimbali ikiwemo kuharisha kutokana uwepo wa Dampo ambalo lipo kandokando mwa Mto Kashai ambapo wanafunzi hao huchota maji kila siku kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kunywa wakiwa shuleni.
ITV imefika katika Dampo hilo ambapo imeshuhudia wanafunzi wakichota maji katika eneo hilo huku kukiwa na baadhi ya vinyesi mbalimbali vya binadamu katika eneo hilo na kushuudia baadhi ya wananchi wakimwaga uchafu katika mto huo huku wanafunzi wa shule ya msingi Kasha wakichota maji ambayo yamekuwa yakitumika kwa matumizi mbalimbali ikwemo kunywa hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kwa wanafunzi hao.
Mkuu wa shule ya Msingi Kashai Lebesi Byangwam amesema eneo hilo sasa limekuwa hatarishi kwa afya za wanafunzi na wananchi wanaolizunguka eneo hilo kwakuwa limekuwa likichangia katika kuchafua chanzo cha mtuo huo ambapo ameiomba serikali kufanya utaratibu wa kuhamisha Dampo hilo haraka ili kunusuru maisha ya wafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Nao baadhi ya wafanya biashara waliopo katika soko la kashai wameonyesha kukelwa na Dampo hilo ambalo sasa limekuwa kikwazo kwa nanchi wanaoishi katika eneo hilo nakwamba serikali isipo chukua hatua za makusudi za kuliondoa Dampo hilo ambalo lipo kandokando mwa mto huo wananchi wataathirika kwa kiasikikubwa napia wamechoshwa na harufu mbaya inayotoka katika Dampo hilo hali ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wananchi pamoja na wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi kashai.
ITV imemtafuta kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya maispaa ya bukoba CHIBUNU LUKIKU bilafanikio kwalengo la kujua kwa kina hatua zitakzo chukuliwa na serikali juu ya kusafisha Dampo hilo na kujaribu kumtafuta kwa njia ya simu ambapo simu yake haikuweza kupatikana.
Next Post Previous Post
Bukobawadau