Bukobawadau

BREAKING NEWS:ZITTO KABWE ATANGAZA RASMI KUACHIA KITI CHA UBUNGE

 Barua ya Zitto Kabwe kwa Mh.Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh.zitto Kabwe ametangaza rasmi kuachia nafasi ya ubunge wa jimbo hilo pamoja na uanachama wa CHADEMA.
Katika maelezo yake kwa mwenyekiti wa shughuli za Bunge muda mfupi kabla ya kuahirisha shughuli hizo usiku huu, Mussa Azzan Zungu, Zitto amesema kuwa leo mchana alimuandikia barua Spika ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile alichodai kuwa ni mgogoro ndani ya chama chake ambacho kimetangaza kumfuta uanachama.
Akisoma barua hiyo Zitto amesema "Hadi muda huu sijapata barua yoyote kuhusiana na hilo lakini inanibidi kuheshimu kauli za viongozi wangu pamoja na chama changu, na kwa mujibu kwa Katiba ya Tanzania siwezi kuendelea kuwa mbunge"
Baada ya maelezo mafupi, Zitto akatangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kuwaaga wabunge wote ikiwa ni pamoja na kuwashukuru kwa ushirikiano na kumalizia kwa kusema kuwa
"MUNGU AKIPENDA TUTAKUWA WOTE MWEZI NOVEMBA"
:-
Next Post Previous Post
Bukobawadau