Bukobawadau

SINTOFAHAMU KATI YA DRAKE NA LIL WAYNE


Msanii wa muziki wa rap nchini Marekani Lil Wayne alikuwa tayari kumshambulia msanii mwenza na rafikiye Drake kwa kumuendea kinyume na mpenzi wake,kulingana na taarifa ya kitabu anachoandika.
Jarida la TMZ nchini Marekani,lilipata taarifa ya mapendekezo ya kitabu hicho ambayo yametumwa katika wachapishaji kadhaa.
Wayne anadai kwamba wakati alipokuwa akihudumia kifungo chake jela katika kisiwa cha Rakers kwa kumiliki bunduki bila kibali.
Inadaiwa kuwa Drake alimtembelea akiwa jela na kukiri mbele yake kwamba ali lala na mpenziwe.
Lil Wayne alisema :Hiki ni kitendo ambacho mwanamume ambaye yuko jela hapendi kusikia kwa sababu ni mungu anayejua ni nini ningelifanya iwapo ningekuwa nje.
Wayne alikiri katika mapendekezo hayo kwamba yeye na mpenziwe walikuwa wakigombana sana ndipo Drake akamwambia kwamba alilala naye.
Hatahivyo Wayne anasema kuwa mwanamke huyo alimwambia kwamba alifanya mapenzi na Drake siku moja kabla ya kukutana na Wayne.
Next Post Previous Post
Bukobawadau