HARUSI YA KIAINA NCHINI MISRI !
Maharusi nchini Misri wameamua
kufanya dhihaka kwa yanayoendelea Ulimwenguni na vitendo vya muuaji
ambaye ni chinja chinja asiyeishiwa na kiu ya damu za watu wasio na
hatia almaarufu ulimwenguni Jihad John ama Mohammed Emwazi,na wameamua
kujitia kwenye tundu la chuma wakiwa na mwanamume anayepunga kisu hewani
ikiwa ni namna ya mtindo wa kusherehekea harusi yao.
Harusi hiyo
ya aina yake ilikuwa ikichukuliwa mkanda wa video,ilitukia eneo la
Menoufia, nchini Misri huku mwanamume huyo apungaye jibisu hewani,uso
ukiwa umevalishwa soksi maalum, akawaongoza wageni waalikwa kuingia
shughulini, kisha akawaongoza maharusi kwenye kibweta cha chuma ama
kisanduku basi kizimba itoshe hapo, sawa alivyowekwa yule rubani Mu'ath
Al Kassasbeh wa nchi ya Jordan kisha akachomwa akiwa hai mwezi wa
February si unakumbuka? Baasi ,mwenye jibisu mithili ya Jihad John
akaamuru wimbo wa kijihad upigwe ambao ulitungwa na wanamgambo wa dola
ya kiislam,ukapigwa.
Ndani ya hicho kizimba maharusi wapya
wakaangusha densi ya nguvu kwa raha zao akiwemo mwanamume aliyeziba
usowe, huku nje ya kizmba wageni waalikwa wakihanikiza kwa makofi na
vigelegele kuwachagiza maharusi wajiachie na kufurahia siku yao muhimu
maishani .
Wazo la kutafuta kizimba na hali ya kijihadi aliitoa
bwana harusi,na alimtaarifu mkewe kuwa anamuandalia kitu tofauti kabisa
na ndoa za watu wengine, akamtaka ajiandae kwa mshangao!
Ni bwana
harusi pekee, wahudumu wa harusi hiyo akiwemo mpiga picha bwana , Ahmed
Kassem, waloujua mpango huo kabla ya siku ya shughuli yenyewe.
Kabla
ya kizimba kufunuliwa, wageni waalikwa walitaharuki wakiamini kuwa
harusi imevamiwa na kundi la kigaidi la dola ya kiislamu IS, mashuhuda
wanaeleza hivyo.
Lakini mwezi uliopita, zilioneshwa picha za mnato
na za video zikionesha wa Misri wa madhehebu ya kikristo ya Coptic
wakichinjwa na kundi hilo huko Libya.
BBC