Bukobawadau

KIJANA MWENYE TATIZO LA ULEMAVU AFUNGIWA NDANI ZAIDI YA MIAKA 10


Kijana mwenye tatizo la ulemavu amegundulika kufungiwa ndani ya chumba kwa zaidi ya miaka kumi na wazazi wake kwa madai ya kuficha aibu bila kutolewa nje kupata hewa katika chumba kilichopo mtaa wa uwazi kata ya kangarawe wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
ITV ilifanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo kabla ya kwenda na camera yao na kuakikisha kuwa kijana huyo ambaye amejulika kwa jina la Hamza Abdalah mwenye umri wa miaka 22 akiwa katika chumba hicho kwa zaidi ya miaka kumi bila kutolewa nje huku akijisaidia katika chumba hicho ambapo licha ya baadhi ya viongozi wa mtaa huo kupata taarifa hizo, wamelalamikia wazazi wa kijana huyo kwa kuficha ugonjwa wa mtoto wao kwa zaidi ya miaka 10 bila kuweka wazi ili jamii iweze kusaidia.

ITV ilipoonana na wazazi wa kijana huyo bwana Abdalah Amri na mkewe, walikiri kumfungia kijana wao kwa miaka mingi, huku wakijitetea kuwa wameishiwa fedha kutokana na matibabu yake.

Aidha viongozi hao pamoja na timu ya ITV tulilazimika kumtoa kijana huyo nje ili aweze apate hewa kuliko kuendelea kukaa katika chumba hicho chenye harufu mbaya.

CREDIT ITV
Next Post Previous Post
Bukobawadau