Bukobawadau

MASHINDANO YA NANI MKALI YAENDELEA KUCHUKUA KASI !

Msimu wa pili wa mashindano  ya 'NANI MKALI'  yanayo andaliwa na TESSO BOY Entertainment  yameendelea tena kufanyika mwishoni mwa juma hili katika fukwe za Kiroyera Mjini Bukoba..
 Mmoja wawasanii maarufu kwa jina la 'Kirokoroko' akiwajibika katika jukwaani katika mchuano wa 'NANI MKALI' unao endeea kuchukua kasi Mjini hapa kwa kuwakutanisha Vijana mbalimbali wenye vipaji tofauti kwa lengo la kutafuta nani Mkali wao

 Mkali  wa miondoko ya Ragga na Dancehall akifanya yake jukwaani
Ndivyo anavyo onekana pichani Jaji kiongozi wa mashindano hayo.
Wasanii wakiendelea kuwajibika
 Ni Wasanii na Vipaza...!
 Taswira mbalimbali kutoka viwanja vya fukwe za Kiroyera katika shindano lake la Nani Mkali lililofanyika jumapili ya jana March 15,2015
 Kushoto ni mshiriki wa  mashindano hayo akiwa jukwaani na Mzazi wake .
Sehemu ya Umati wa watu wakati mashindano yakiendelea kufanyika
Msanii anayefanya vyema katika michano Michano (The Mic King)  mara baada ya kushuka jukwaani kushiriki mashindano ya 'Nani Mkali' yaliyofanyika jumapili ya jana katika viwanja vya fukweni Kiroyera.
 Mmoja wa Mc Muongozaji wa mashindano hayo
 Umati mkubwa ukifuatilia mchuano wa wasanii wanaotikisa katika fani mbalimbali Mji hapa
Wachaa Kabisa....!

Meza ya Majaji wa Shindano la 'Nani Mkali' katika Uigizaji,kuimba na kucheza.

 Meza ya Wadau wakubwa katika tasnia ya burudani , Shangwe na Kadansee Mjini hapa.
TESSO BOY Entertainment ambao ndio Waratibu na waandaaji wa Mashindano ya 'Nani Mkali' katika tasnia ya kucheza muziki ,kuimba na Uigizaji mkoani Kagera wanasema fainali za  mashindano haya yanayo endelea kila siku za Jumapili  itafanyika siku ya Pasaka katika Viwanja vya fukweni Kiroyero Mjini hapa.
Mdau pichani kushoto akiwa na muandaji wa mashindano hayo Mpambanaji  Tesso Boy 
 Meza ya Majiji katika mashindano hayo.
 Mkali katika Miondoko ya Hip hop akiimba Accapella na freestyle kama vile Kendrick Lamar 
 Mmoja wa washiriki akiendelea kuonyesha uwezo wake jukwaani
 Mzee wa 'Kirokoroko' msanii aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia 'Nani Mkali'
 MWISHO wa Matukio ya picha yaliyojiri Jumapili hii katika Viwanja vya fukweni Kiroyera katika Shindano la Nani Mkali.

Next Post Previous Post
Bukobawadau