Bukobawadau

NONDO KWA JUMATANO YA LEO MARCH 18,2015

Watoto kwenye ndoa sio chanzo cha furaha, na wala hawaji kuleta furaha bali wanakuja kuongeza na kuendeleza furaha iliyokuwepo baina yenu ninyi wapenzi. Ukiona mtu anasema watoto wameleta furaha maana yake haikuwepo awali. Watoto hawawezi hata sikumoja kuchukua "kureplace" nafasi ya furaha ya ndoa, ndoa inafuraha yake na watoto wanafuraha yao, vyote hivi vinaleta ukamilifu wa furaha ya kweli. Inauma sana pale furaha ya ndoa inapokufa na mtu anabaki tu kwa ajili ya watoto, inasumbua moyo sana pale mtu anapoona hapati tena furaha kutoka kwa mume au mke wake na anaamua kuhamishia mapenzi kwa watoto. Utamu wa asali ni wa asali na utamu wa sukari ni wa sukari ingawa vyote ni vitamu na vyote hutumika kwenye chai, kimoja kimetoka kwenye mmea na kingine kwenge mdudu. Jifunze kutofautisha na kuiheshimu tofauti iliyopo.
 Mara nyingine kwenye mahusiano mmoja anaweza kuamua kuanzisha mazingira ya ugomvi ili tu hali ya hewa ichafuke yeye apate upenyo wa kutoka na kwenda kwenye mchepuko au kwenye mishemishe nyingine. Kikawaida ni ngumu kuamua kuondoka kwenda kumsaliti unayempenda wakati anakuchekea na kila kitu baina yenu kiko sawa, hii inaitwa "guilty conscious" ingawa wako ambao hawana hiki kitu na wanaweza kukusaliti katikati ya kipidi cha amani na furaha tele. Sasa wengi hutumia mbinu inaitwa "chafua hewa utoke", yamkini hata haendi kwa mwanamke bali anaenda kwa marafiki zake au kwenye kinywaji na anajua wewe ni kipingamizi cha kutoka kwake basi anaamua kuchafua hali ya hewa ili asepe. Sasa basi maranyingine ukiona mwenzako anakuvuruga mivurugo isiyo na sababu kabla ya kumuuliza "kwanini unafanya hivi ?", muulize " unataka kwenda wapi?" - Chris Mauki
Next Post Previous Post
Bukobawadau