Bukobawadau

SONGEA:MWANAMKE ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMKATA MTOTO KWA JEMBE JICHONI

Mwanamke mmoja Shida Ngai mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa makambi katika manispaa ya Songea mkoani ruvuma, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga na kisha kumkata kwa jembe kwenye jicho la kushoto mtoto wa kaka yake Daudi Ngai mwenye umri wa miaka 17 kwa kosa la kukanyaga nguo zilizokuwa zikifuliwa. Mtoto Daudi Ngai anayeishi na shangazi yake huyo Shida Ngai, baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia kwa kuumwa, akizungumza na ITV amesema alikanyaga nguo iliyokua ikifuliwa na mtoto wa shangazi yake kwa bahati mbaya lakini adhabu aliyoipata ni kubwa mno na kwamba mbali ya kupata manyanyaso ya kila siku na shangazi yake huyo lakini pia amekuwa akimtishia kumpa sumu ili afe na kufuata wazazi wake. Mtuhumiwa Shida anasema yeye alichukua jukumu la kumpiga mtoto huyo kutokana na hasira huku akikana kwamba hajampiga kwa jembe kama inavyotajwa. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma,Mihayo Msikhela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hatua zaidi za kumfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake zinaendelea kufanyika
CHANZO ITV.
Next Post Previous Post
Bukobawadau