Bukobawadau

WATANO WAJERUHIWA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI JIJINI MWANZA

 Watu watano wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa Bugando, baada ya kuangukiwa na kifusi cha ukuta wa jengo la biashara la Ghorofa saba linalojengwa katika eneo la barabara ya nyerere jijini Mwanza, huku askari wa kikosi cha zimamoto na uokoaji,polisi na mgambo wa jiji wakiendelea kumtafuta mtu mmoja anayedaiwa kufukiwa ndani ya shimo lenye urefu wa zaidi ya mita tatu.
Hali ya Majeruhi katika hospitali ya rufaa Bugando,majeruhi waliolazwa katika idara ya dharura zinavyoendelea, ambapo Daktari wa zamu katika idara hiyo Dk. Ernest Elisenguo amesema majeruhi wawili, Benson Daud na Ramadhan Mkumba hali zao haziridhishi.
 Muda mfupi baada ya ukuta huo kuanguka na kusababisha majeruhi, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya nyamagana,ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Baraka Konisaga imewasili katika eneo hilo na kutoa agizo kwa uongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza.
 Eneo hili la ndani ambapo askari wa Zima Moto na uoakoaji wakiwa kazini kuvuta maji ili kuangalia vibarua wengine waliokuwa wakichimba kama wapo ndani hai au maiti, hii ni baada ya kuwaokoa watanowakiwa majeruhi  vibaya baada ya kuanguka kwa ukuta wa jengo la biashara lililopo kitalu namba 6, block ‘U’mtaa wa Nyerere, linalojengwa na mkandarasi kampuni ya HYSCON ENGINEERING LTD YA Mwanza.
Next Post Previous Post
Bukobawadau