Bukobawadau

MAUAJI YA KUKATA KOLOMEO :WATU SITA WASHIKILIWA NA POLISI MKOA KAGERA

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limewatia mbaloni watu sita akiwemo na mganga wa kienyeji moja anaedaiwa kufadhili vitendo vya mauaji ya kunchinja watu na kuondoa badhi ya viungo na wengine wawili kupigwa lisasi hadi kufa walipokuwa wakijalibukutoka mikononi mwa polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera ACP Henry Mwaibambe amesema jeshi la polisi sasa linandelea na msako mkali ambapo ameongeza kuwa sasa limebaini mtandao wa watu hao wanaojihusisha na matukio hayo nakufanikiwa kukamata watu sita pamoja na mganga wa jadi mmoja anaedaiwa kuwafadhili watu hao kwa kuwapa tunguli na irizi iliwaweze kufanya matukio hayo ya kinyama nakwamba kati ya watuhimiwa hao sita wawili wamefariki dunia kwa kupigwa risasi akiwemo kinara wa mauaji hayo wakati wakijaribu kutoroka mikono mwa polisi. 
Next Post Previous Post
Bukobawadau