Bukobawadau

'OMWANA RUKIA' WA BASHIR ALIVYO AGWA !!

Hii ilikuwa pale Linas Night Club jumapili ya Juma lililopita April 19,2015 ukweli ni kwamba ni kati ya Sherehe iliyopendeza sana na kuvutia zaidi kwani watu wake walitoka bomba, waling'ara ile mbaya,Shangwe za kutosha ukumbini, mpangilio mzuri ,zawadi za kutosha kama itavyo onekana katika muendelezo wa matukio kwenye picha  na sehemu ya Video.
 Kivutio kikubwa ni Mbwembwe na vikeleshendo wakati Mhusika Bi Rukia Nadhir wa Bashir akiingia ukumbini na wake wa ubani Mr Bashir Kabyemela, wakionyesha ufundi katika kucheza.
 Kasi ya wadau wakichukua matukio kwa simu zao

 Naam ni mikato na Swaggar wakati wanaingia ukumbi
 Sehemu kubwa ya waalikwa wanaonekana kufurahi na kuwashangilia sana.
 Mwanzo alitangulia Binti wa kusafisha njia pichani aliye onyesha umahiri wake katika kucheza kwa style ya kutikisa nyonga akiwaoneshea waalikwa ukumbini.
Wallah hatuna namna ya kuelezea Style za uchezaji ,kikubwa ni Shangwe na mayowe vilivyosikika kutoka kwa waalikwa ukumbini
 Wapambe wakiwa nyuma yake wakati akiingia ukumbini
 Mhhh !! Kwa Ishara za vidole hatuna neno
Kwa furaha kubwa anawapungia watu Mikono akiwa anaingia ukumbini
Muonekano sehemu ya Waalikwa ndani ya ukumbi wa Linas Night Club
 Naam Bw.Bashir na Bi Rukia LIVE wanalishana keki kwa style ya njiwa!
 Hakikailikuwa ni furaha tupu kwa wawili hawa...!
 Ndugu wa Bwana Bashir Kabyemela wakifuatilia kinacho kwa ukaribu.
Wakiwa na furaha kumpokea Mama Bashir Kabyemela
 'Nani kama Mama'
 Rukia wa Bashir anamlisha mama mkwe wake (Ma Zamda Abdallah Kabyemela) kipande cha keki.
Naam Mama Amina Sued Kagasheki, Mama Mzazi wa Bi Rukia anapokea kipande cha Keki.
 Umati wa watu ukumbini unaonyesha kufurahia kinacho endelea.
Mama Chichi /Mrs Abubar Sued pichani kulia akifanya kusasambula.
 Anaonekana mwenye furaha pichani ni Mama Achi ,Wifi yake Bi Rukia
 Mama Farida akitoa neno la shukrani kwa waalikwa wote ukumbini na kuwashukuru wanachama wake kwa michango yao,Yeye ni sehemu ya mzazi wa Bi Rukia (Mke wa mjomba )
 Waalikwa na wanafamilia wakiendelea kutoa zawadi kwa Bi Rukia
 Sehemu ya wanafamilia wakiendelea kukabidhi zawadi zao
 Mrs Jumanne Bingwa akifuatana na Binti yake Jaharia
 Zawadi mbalimbali kutoka kwa mama mkwe ilikiwa ni pamoja meza ya kioo (Dressing table)
Ukumbini ni mwendo wa Rusha roho na Miduara
 Wanawake wakicheza kwa kushangilia
Wanaonekana Mawifi zake Bi Rukia wakati utambulisho.
 Bi Skitu wa mbele pichani ndiye Mshonaji  maridadi wa Gauni alilovaa Bi Rukia Nadhir wa Bashir.
Mama Amina Sued Kagasheki (kushoto) Mzazi wa Bi Rukia akitabasamu  kama uonavyo pichani
 Mama Mzaa Chema akiwa na mwanae
 Katika picha na Wasafisha njia
Kwa furaha na tabasamu pana hakika amependeza !
 Sehemu ya zawadi zilizotolewa na Mama Mzazi wa Bi Rukia
 Kumbuka Matukio zaidi ya picha 150 yanapatikana katika ukurasa wetu wa facebook
 Mkono wa pongezi na zawadi  kutoka kwa waalikwa
 Sehemu ya zawadi kutoka kwa Mama Mzazi Mama Amina Sued Kagasheki.
 Kwa ukaribu mkubwa kama upande wa pili wa Mzazi pichani ni Mama Khajali (Mama Moha)
 Mc Mahiri wa shughuli hii anatanabahisha kiasi cha fedha taslim kilichopatikana kutoka kwa Wanakamati na Waalikwa Ukumbini.
Mama Aisha na Mama Khajali nao mdogo mdogo na zawadi walizo ziandaa kwa ajili ya Bi Rukia.
 Wajukuu wa Mama Amina nao wakafanya yao.
 Bi Maua kama kawaida
 La Familia hao ni Kabyemela's kutoka pande za Maruku
Shangwe za hapa na pale ukumbini
 Muendelezo wa picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
Katika ukodak na Shost wake wa karibu

 Katika pozi anaonekana Bi Rukia mke wa Bwana Bashir Kabyemela
Katika picha ya kumbukumbu na Vijana ambao ndio wamesimama kama wapambe wa Bi Rukia.
Wawili hawa wakati wanaingia ukumbini kwa kusakata rumba 'Ebyehatari'
 Ile nyimbo yenye maneno yasemayo "Mapenzi hayana ubaunsa wala ukomandoo" hapa ikahusika
 EVENT ::KITCHEN PARTY
BRIDE ::RUKIA
VENUE ::LINAS CLUB
PHOTO ::BUKOBAWADAU
COLOUR ::PINK & BLACK
DESIGNER::SIKITU FASHIONS
Hakika "Umependeza mno Bibie"

Matukio ya picha zaidi jiunge nasi katika ukurasa wetu wa FB, gonga hapa>>>BUKOBAWADAU MEDIA

Next Post Previous Post
Bukobawadau