Bukobawadau

UPDATE:SAKATA LA BASTOLA YA MH. AMANI!

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Mjini Bukoba ni kwamba Mh . Anatory Amani ameachiliwa huru baada ya kuwa ameshikiliwa kwa masaa kadhaa kutokana na sakata la bastola yake,Modeli mashuhuri ya mwanzoni kabisa aina ya 'Groovy' kupotea katika mazingira yenye utata.

Mh. Amani alifika Polisi kutoa taarifa ya kupotelewa na bastola yake anayoimiliki kihalali toka mwaka 2006 ,baada ya kupokea maelezo kutoka kwake ,Jeshi la polisi likamuweka ndani kwa ajili ya uchunguzi juu ya tukio hilo.


Baada ya uchunguzi taarifa zinasema kwamba mmoja wa wajukuu wa Mh. Amani aitwaye Justine Mwijage mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Peace inamilikiwa na Dk Amani amekamatwa ta bastola hiyo.
Inasemekana kijana huyo amekamatiwa Wilayani Geita siku ya leo,taarifa inasema Mh. Amani akiwa safarini ,kijana huyo alipata fursa ya kuvunja Chumba na kutoweka na silaha hiyo ya moto ndogo yenye kasiba fupi inayoshikwa kwa mkono mmoja.
Mpaka tunaingia mitamboni kijani huyo bado yupo mikononi mwa Polisi!
Next Post Previous Post
Bukobawadau