Bukobawadau

WEMA ATOA SABABU ZA KUFUNGA NDOA YA SIRI!

 Wema Sepetu amefunguka kuhusu Picha zake alizo post siku mbili zilizopita akionekana ndani ya vazi la Harusi/ shela, Wema amedai kwamba Picha hizo ni za Ndoa yake ya siri iliyofanyika hivi karibuni Bomani na ndoa yake imefungwa ki serikali kwa sababu bwana harusi ambaye hakua tayari kumtaja jina dini yake ni Mkristo wakati yeye Wema ni muislam na ndoa hiyo ilihudhuriwa na idadi ya watu wasiozidi watano, na picha alizo post kwenye mtandao zimepigwa katika hoteli ya Double Tree jijini dar es salaam ambako kulifanyika hafla fupi.
 Akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa aliamua kufunga ndoa ya siri kwa kuogopa kupigwa ‘juju’ na mumewe kushindwa kumuoa.
"Mume wangu ni Mtanzania na siyo maarufu na ndoa yangu ilihudhuliwa na ndugu zangu wachache na ndugu wa mume wangu sikutaka watu wengi niliogopa kupigwa juju na mume wangu asingenioa,"alisema Wema.
Alipoulizwa kuhusu tatizo lake la kutoshika mimba mumewe alilichukuaje alisema kuwa hana tatizo naye na amekubali kuishi hivyo hivyo.

Wema akaendelea kutoboa kuwa wanampango wa kusafiri hivi karibuni huenda ikawa nje ya nchi kwa ajili Honey Moon, Wema ameolewa na mwanaume mwenye umri wa kati si kijana si mzee na hajaolewa ndoa ya mitala, yeye ndiye mke wa kwanza kwa mwanaume huyo
Chanzo: CloudsFM
Next Post Previous Post
Bukobawadau