Bukobawadau

CHANGAMOTO MABORESHO USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA ZATAJWA

Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbaliMsemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani. Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP. Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP.[/caption] PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake. Mratibu wa Mradi huo ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo. Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi. Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu. Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma. Mradi pia umefanikiwa kuimarisha ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini, kutumika kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya kuingiza mahitaji ya Mpango wa miaka mitano na kugawa rasilimali na pia kuchapishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali hivyo kuongeza kiwango cha uwazi. Mengine ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 badala ya sheria iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo mengine imeiweka PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi, na kubaki na shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma. Vile vile sheria imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya ununuzi wa umma. "...Kujenga uwezo wa watumishi katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Kwa mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu, wakaguzi, wachumi; maafisa wa ununuzi...kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kulitumikia taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya mfumo wa IFMS ili kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa mfumo wa kusimamia mali za serikali (Asset tracking software) katiak ofisi zote za kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali." Alisema Mratibu huyo. Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua ya 3 ya AFROSAE, uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5 ulibadilishwa na kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi kuliko ule wa mwanzo, Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda serikali za mitaa na kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa fedha toka serikali kuu kwenda kwenye LGAs. Mratibu alibainisha kwa sasa Ofisi ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo wa IFMS, na hivyo kuongeza ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya kimataifa ya International Public Sector Accounting Standards Cash Basis (IPSAS). Mradi wa PFMRP ulianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika serikali na taasisi zake, huku ikitekelezwa sambamba na programu nyingine za kitaifa katika sekta ya umma. *Imeandaliwa na www.thehabari.com ____________________________________________________ Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau