PROF TIBAIJUKA ACHANGIA MIL 60 KUKUZA MITAJI YA WANAWAKE JIMBONI MWAKE
Zaidi ya vikundi 500 vya
wajasiliamali kutoka kata 17 kati ya 25 zinazounda jimbo la Muleba Kusini
Mkoani Kagera vimepokea mchango wa Sh 60 milioni kutoka kwa mbunge wa jimbo
hilo kwa lengo la kuboresha mitaji na kujipanua kiuchumi
Akihutubia wawakilishi wa
vikundi hivyo jana katika ukumbi wa Kajumulo Foundation mjini Muleba mbunge
wa jimbo hilo Profesa Anna Tibaijuka amesema vikundi alivyochangia fedha hizo
ni vya wanawake , Vijana pamoja na wazee
Profesa Tibaijuka amesema kuwa
vikundi hivyo ni vile vilivyopata usajili kupitia idara ya ushirika wilayani
humo na kutimiza masharti ya kuanzishwa vikundi vya ujasiliamali hivyo
anaviongezea mitaji viweze kupanuka na kujipatia maendeleo.
Aidha amesema katika ziara yake ya
Mwezi Machi hadi April kuzungukia wapiga kura alikabidhiwa risala za
vikundi hivyo kwa kutajiwa changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa mitaji, elimu
ya ujasiliamali pamoja na kukosa masoko.
“Wananchama wa vikundi hivyo
hawana budi kuwa wabunifu katika kuendesha vikundi hivyo ambapo halmashauri ya
wilaya iendelee kutafuta fedha kutoka vyanzo vya ndani kusaidia vikundi vya
vijana na wanawake”Alisema Tibaijuka
Viongozi wa vikundi wamepongeza
kuhusu juhudi za mbunge huyo ambaye hakubagua jografia ya jimbo hilo kwani
kahusisha kuchangia vikundi hata vile vilivyoko visiwani ambavyo wajumbe
wake wanaishi mazingira magumu
Kwa upande wake diwani wa kata ya
Gwanseli (CUF) Julius Rwakyendela amesema kuchangia vikundi hivyo ni wajibu
wake na kwamba alichelewa kuwakumbuka wananchi labda ni kwa nafasi
aliyokuwa nayo ya uwaziri.
Amesema katika kata yake amechangia
kikundi cha vijana wanaotengeneza barabara kwa mikono ambayo alipita na
kushindwa kufikia baadhi ya vijiji kutokana na miundombinu hafifu ya
kuharakisha maendeleo ya kijamii.
Pamoja na hayo Mwenyekiti wa CCM
wilayani Muleba Muhaji Bushako ambaye ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo
la Muleba Kusini amebeza uchangiaji wa vikundi akidai ni takrima ya
kutaka kujisafisha kwa wapiga kura
Bushako amesema kinachofanyika ni
kujinadi kwa kila kijiji kuendelea kuwatumikia wana jimbo lakini muda wake
ameupoteza akiwa Waziri na kufanya zaidi shughuli za kitaifa akiwasahau
wapiga kura aliowawakilisha bungeni.
Wanawake hao pia waliweza kupata chakula pamoja na mh
Tibaijuka baada ya kuhakikisha wamepata fedha ambapo vipo vikundi vya
kilimo cha mboga mboga mazao ya chakula na biashara vikundi vya biashara
ndogo ndogo na vijana wa nguvukazi ya kupambana na kung'oa migomba
yenye mnyauko na utengenezaji wa miundombinu ya barabara ili kupatikana
huduma bora ndani ya jamii
Vikundi vya akina mama na wazee ni
pamoja na vile vya kuweka na kukopa kisha kutoa elimu ya akiba na mikopo
kutoka idara ya ushirika kwa lengo la kugawana faida na kuendeleza
maisha yaoTaarifa zinazo husiana na Mama Anna Jimboni mwake ingia hapa > WAHITIMU MAFUNZO YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI KWA UDHAMINI WA MAMA ANNA