Bukobawadau

SERIKALI YATAKIWA KUHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI UPIGAJI KURA UCHAGUZI MKUU

Kulia mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo. Kulia mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa. Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa.Kushoto mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers). Kushoto mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers).Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.  Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) wakiwa katika semina hiyo. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) wakiwa katika semina hiyo.washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo. washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo. washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
Na Joachim Mushi, WANAHARAKATI Ngazi ya Jamii nchini wametoa madai kuelekea Uchaguzi Mkuu huku wakiiomba Serikali iharakishe mchakato wa uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura ili vijana wengi wanaostahili waweze kuitumia haki yao ya msingi ya kushiriki mchakato wa uchaguzi na ule wa kura ya maoni. Madai hayo yametolewa katika tamko lao lililotolewa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) kwenye warsha ya majadiliano kati ya waandishi wa habari, wachora katuni na waandishi wa habari za mitandao ya jamii iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katika madai hayo wanaharakati ngazi ya jamii pia wameomba elimu ya uraia na ya mpiga kura itolewe kwa wingi ili iwafikie vijana wapate hamasa ya kujitokeza kugombea na kupiga kura, ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waweze kupata nafasi sawa kama wagombea kwenye uchaguzi bila upendeleo wala woga. Aidha imetaka vijana wanaojitokeza kama wagombea wawekewe mazingira rafiki ikiwezekana wapewe ruzuku ya kuwasaidia kushindana kwenye uwanja wa demokrasia, pamoja na kushauri Sera ya Taifa ya Vijana pamoja na Mkataba wa Vijana wa Afrika unalitambua kundi la vijana kama rasilimali mojawapo muhimu sana kwenye maendeleo na pia katika kulinda amani na utulivu kwenye Bara la Afrika. "...Hata hivyo pamoja na kwamba vijana ni zaidi ya 60% bado mchango na thamani ya vijana haujatumika ipasavyo kwenye demokrasia ya Tanzania, huku thamani yao ikionekana tu nyakati za uchaguzi kwa kutumiwa kama walinzi au wapambe wa wagombea," imeeleza sehemu ya tamko hilo. Limebainisha kuwa pamoja na uanzishwaji wa Mabaraza ya Vijana kwa vyama vingi, mengi hayana nguvu ya maamuzi kwa kuingiliwa na vyombo vya juu vya Chama, ikiwa ni pamoja na kukumbusha kuwa mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka ambao vijana wengi waliingia Bungeni na wamekuwa chachu kubwa ya kuchangia na kuibua mijadala yenye tija Bungeni. Hata hivyo imeeleza kuwa bado idadi ya vijana wanaojitokeza kupiga kura hasa wasichana bado ni ndogo ukilinganisha na ile ya wanaojiandikisha na wanaoshiriki kwenye kampeni, vijana wengi wanaojitokeza kwa kuweka nia ya kugombea wamekumbana na kigingi cha uteuzi kwa kutokubalika ndani ya vyama kwa mawazo mgando kwamba umri wao hauwawezeshi kufanya uchambuzi wa masuala makubwa ya kitaifa, kadhalika changamoto ya nguvu yao ndogo kiuchumi ajira ambayo inawafanya wasiweze kushindana kikamilifu katika uwanja usio na usawa wa siasa. Kwa upande wa vyama vya siasa tamko hilo limetaka watu wenye ulemavu waingizwe kwenye sera na mipango ya nchi kwa vitendo kwani bado ushiriki wao kwenye masuala ya uchaguzi na uongozi uko chini. Madai mengine ni pamoja na Vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kuhakikisha zinazingatia ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye uchaguzi kama wagombea na wapiga kura, Serikali kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu ili washiriki kikamilifu kwenye michakato yote ya maendeleo, hii ni pamoja na uchapishaji wa sheria na kanuni kwa lugha rahisi ikiwemo maandishi ya nukta nundu, vituo rafiki vya kampeni na kupiga kura kwa watu wenye ulemavu. Mengine ni pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi, kudai ulinzi na usalama wa maisha yao, kama raia wa taifa hili, uwepo wa mikakati ya kuelimisha umma uondokane na mawazo potofu yanayoashiria kutishia uhai na usalama wa kundi hili na hasa wenye ulemavu wa ngozi. Hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaohusika. "...Serikali ihakikishe upatikanaji wa taarifa na maarifa kwa njia rahisi ikiwemo lugha ya alama na maandishi ya nukta nundu kutoa elimu ya mpiga kura na pia vyombo vya habari kama vile TV ziweke wakalimani hasa katika vipindi vya taarifa ya habari na vipindi vyote vyenye mijadala ya kitaifa. Mgombea tutakayempa kura ni Yule ambaye miongoni mwa sera zake itakua ni kupinga ukatili wa kijinsia kwa hali zote bila woga wala upendeleo Aidha mengine ni pamoja na Serikali itakayoingia madarakani kuhakikisha inaunda Tume ya Kughulikia Ukatiki wa Kijinsia kama zilivyo Tume nyingine, kuunda mahakama maalum ya kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia ngazi ya familia na kuweka mikakati halisi ya kuhakikisha kwamba kila mwanamke ana haki ya uchumi na haki ya maisha endelevu/ajira akiwa kijijini au mjini, mwenye ulemavu, mzee au kijana, wanawake na wanaume wote wapate kipato kinachotosheleza kuishi maisha bora kama binadamu. Warsha hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) imejumuisha makundi mbalimbali ya wanahabari ikiwa ni lengo la kuwajengea uwezo kuandika masuala ya kijinsia kwa kina. *Imeandaliwa na www.thehabari.com ------------------------------------------------------------------------------------------------------------- Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470 Web:- www.thehabari.com http://joemushi.blogspot.com
Next Post Previous Post
Bukobawadau