Askari saba wa Jeshi la Polisi
nchini, kitengo cha Usalama Barabarani, wamenusurika kifo kufuatia ajali
iliyohusisha gari la Polisi na gari moja binafsi mjini Arusha leo hii.
Gari zilizohusika katika ajali hiyo, zote ni aina ya Toyota Land
Cruiser, moja likiwa ni mali ya Jeshi la Polisi nchini, na jingine lenye
namba T 549 ADM, ambalo ni mali ya kampuni moja ya Utalii mkoani humo.
Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo, kupitia
taarifa fupi iliyopatikana kwenye mtandao wa kijamii unaoendeshwa na
Mabalozi wa Usalama Barabarani, taarifa ya Jeshi hilo imesomeka kama
ifuatavyo;
Ni kweli ajali imetokea na kusababisha majeruhi 7 wakiwa ni askari wa
U/barabarani Arusha. Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva hatimaye
kushindwa kumudu gari na kusababisha gari kuhama lane nyingine na
kugonga gari la Polisi lililokuwa linakuja mjini Arusha. Dereva alikuwa
amelewa na kwa kiwango kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa
Serian hospita kwa matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu
wamelazwa na wanaendelea vizuri.
Hii ndio hali halisi ya tukio la kugongwa kwa hao trafiki huko arusha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment