Bukobawadau

Dk.Shein achukua fomu ya Urais Z'bar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha mkoba wa wenye fomu kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa Fomu hizo katika Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo Juni 18,2015.[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipozungumza na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo alipofika  kuchukua fomu za kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar,(kushoto)Mama Mwanamwema Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia)Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Unguja Haji Juma na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar VuaiAli Vuai.
 Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakisherehekea wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokwenda kuchukua fomu kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwanndui Mjini Unguja leo.
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau