Bukobawadau

DOZI YA LEO:WEWE NI BABA JINA AU BABA MAJUKUMU???

Fatherhood is not claimed by words but action, kukubalika na kuheshimika kama baba nyumbani kwako hakuji kwa kuwalazimisha wanao na wote waishio ndani kwako wajue kuwa wewe ndiyo baba wa nyumba bali kwa matendo halisi yanayotegemewa kila baba kuyafanya. Sasa unakuta mwanaume mzima hafanyi yale ambayo baba anatakiwa kufanya, watoto au wengine hapo ndani wakiihamishia heshima kwa mama au mtu mwingine utasikia mtu anaanza kung’aka. Ngoja nikwambie, watoto wadogo hata kama wana umri mdogo huwa wanajua majukumu yanayotegemewa kutoka kwa baba au mama, sasa mmoja asipofanya majukumu yake watoto, dada wa kazi, kaka wa kazi au wengine huwa wanajua. Ukiona mwanaume amefikia kujitambulisha kwa watoto wake kuwa “mimi ndiyo baba wa hii nyumba, hakuna baba mwingine hapa” ujue kashashindwa kazi huyo - Chris Mauki
Next Post Previous Post
Bukobawadau