HAFLA YA UFUNGAJI RASMI WA KAMBI YA WATOTO (ARIEL CAMP )ILIYOANDALIWA NA SHIRIKA LA AGPAHI MJINI BUKOBA JUNE 19,2015
Mgeni Rasmi katika ufungaji wa kambi ya watoto (Ariel Camp) iliyoandaliwa na shirika la AGPAHI, Mh. John Mongella akiwahutubia waalikwa na watoto walioshiriki hafla hiyo.
Sehemu ya Watoto wanao hudumiwa na shirika la AGPAHI wakimsalimia Mgeni Rasmi katika hafla ya ufungaji kambi iliyofanyika Ijumaa June 19,2015 katika hoteli ya ELCT Bukoba.
Baadhi ya waalikwa wakati wa utambulisho.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la AGPAHI kutoka kushoto (Liberator Kagenzi na Cecilia Yona)
Sehemu ya Watoto wanao hudumiwa na shirika la AGPAHI wakimsalimia Mgeni Rasmi katika hafla ya ufungaji kambi iliyofanyika Ijumaa June 19,2015 katika hoteli ya ELCT Bukoba.
Baadhi ya waalikwa wakati wa utambulisho.
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la AGPAHI kutoka kushoto (Liberator Kagenzi na Cecilia Yona)
Madaktari kutoka Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania -kutoka kushoto ni Dr. Festo Manyama na Dr. Maimuna Ahmed wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. John Mongella.
Hotuba fupi ya mheshimiwa Mgeni Rasmi John V. K. Mongella
·
Mkurugenzi
Mtendaji wa AGPAHI,
·
Mganga
Mkuu (M) - Kagera,
·
Waganga
Wakuu (M) – Shinyanga na Simiyu
·
Meneja
wa Miradi wa AGPAHI – Shinyanga & Simiyu,
·
Madaktari
kutoka Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania,
·
Wafanyakazi
wa AGPAHI,
·
Walezi
wa Watoto,
·
Wadau
mbalimbali wa Afya na Haki za Watoto,
·
Watoto
wa Kambi ya Ariel,
·
Waandishi
wa Habari,
·
Wageni
Waalikwa,
·
Mabibi
na Mabwana.
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu,
mwingi wa Rehema kwa kutuwezesha
kukutana pamoja siku ya leo. Pia, napenda kuushukuru uongozi wa AGPAHI kwa
kuandaa kambi hii ya watoto na kunikaribisha kushiriki katika siku hii muhimu ya
kufunga rasmi kambi ya watoto iliyofanyika kwa muda wa wiki moja. Ninayo furaha
kubwa sana kuwa nanyi hapa na nachukua fursa hii kuwakaribisheni Mkoa wa Kagera.
Vile vile, ninapenda kuwashukuru wageni
waalikwa kwa kuweza kufika hapa, hii inaashiria kuwa mnatambua na mnathamini umuhimu
wa kuwajali watoto hawa.
Ndugu
wageni Waalikwa,
Nimefahamishwa kwamba, shirika la AGPAHI
lilianza huduma za malezi na kuwakutanisha watoto katika vikundi baada ya
kuanzishwa kwa Shirika lenyewe mwaka 2011. Nawapongeza kwa kuunda vikundi
vidogo vidogo vya watoto katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo hadi sasa,
mmenieleza mna jumla ya vikundi vipatavyo 35 vya watoto kwenye mikoa ya
Shinyanga na Simiyu vyenye jumla ya watoto 1541.
Kutokana na kuundwa kwa vikundi hivi, AGPAHI iliweka
utaratibu wa kuendesha kambi ili kuwakutanisha watoto kutoka kwenye vikundi
mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu afya na stadi za maisha na pia
kubadilishana uzoefu. Pia, kambi hizi huwajenga vijana na kuwafanya mabalozi wa
huduma za watoto katika jamii. Kambi hizi za watoto zimekuwa zikifanyika mara
moja kwa mwaka na kambi hii ni ya Tano kufanyika. Kambi mbili za mwanzo
zilifanyika mkoani Mwanza na kambi ya tatu na ya nne zimefanyika mkoani
Kilimanjaro; na kambi ya tano mkoani Kagera.
Wageni
Waalikwa,
Nimefurahishwa na jitihada hizi za shirika la
AGPAHI kwani zinawajenga watoto kisaikojia na kuboresha afya za watoto katika nyanja
mbali mbali. Kupitia mkusanyiko huu, nawaomba wadau wengine wa afya na haki za
watoto kuiga jitihada hizi, kwa kuwapa huduma stahiki na kuwalea watoto wetu
katika maadili yanayokubalika.
Vilevile, nachukua fursa hii, kuwasihi watoto
mzingatie masomo ikiwa ndio msingi mkuu wa maisha ya baadae. Nimefahamishwa
kuwa, shirika la AGPAHI hivi punde litawapatia mahitaji ya shule ikiwemo sare za
shule na madaftari ili muweze kusoma vizuri. Pia nawaomba mzingatie kanuni za
afya ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa kama mnavyoelekezwa na wataalam wa afya na endeleeni
kuwa wanachama wazuri katika vikundi vya watoto vinavyosimamiwa na AGPAHI.
Natambua kuwa katika kipindi cha wiki moja
mmeweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo - stadi za maisha na mabadiliko ya
tabia kutokana na msukumo wa kundi, taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI, usafi
binafsi, elimu ya ujana, mahusiano na Uzazi wa Mapango, ufuasi mzuri wa dawa,
lishe, jinsi ya kuwasiliana, huduma na msaada wa kisaikolojia. Pamoja na
mafunzo mliyojifunza katika kambi hii, mmeongeza wigo wa jiografia yenu kwa
kusafiri kuja Mkoa wa Kagera na kufanya matembezi ya kwenda kwenye kiwanda cha
sukari cha Kagera, kuona mto Kagera, makumbusho ya vita vya Idd Amin hadi mpaka
wa Tanzania na Uganda.
Pia, napenda kuwashukuru walezi ambao
wamesafiri na watoto kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu. Naomba mpeleke
shukrani kwa walezi wengine waliobaki kwa kazi nzuri wanazozifanya za kuunda
vikundi vya watoto, kuwalea watoto katika maadili mazuri ya kitanzania na
kuwaelimisha juu ya huduma za afya.
Mwisho napenda kuwaaga watoto na walezi na nawatakia
safari njema mnaporudi nyumbani. Pia, nawatakieni masomo mema.
Baada ya kusema hayo machache, sasa napenda
kutamka rasmi kuwa, Kambi ya Ariel mwaka 2015 mkoani Kagera imefungwa.
ASANTENI
KWA KUNISIKILIZA!
MC muongozaji wa shughuli hii Bw. Emilian Ng'wandu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI Bw. Laurean .R.Bwanakunu kwenye ufungaji rasmi wa Kambi ya Ariel.
Afisa Mawasiliano wa
shirika la AGPAHI, Jane Shuma akitolea jambo ufafanuzi.
Hotuba
fupi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la AGPAHI Bw. Laurean .R.Bwanakunu kwenye
ufungaji rasmi wa Kambi ya Ariel, leo Ijumaa June 19,2015
Ndugu,
·
Mgeni Rasmi, Mkuu
wa Mkoa wa Kagera,
·
Mganga Mkuu (M) -
Kagera,
·
Waganga Wakuu (M)
– Shinyanga na Simiyu
·
Madaktari kutoka
Chama cha Madaktari wa Watoto Tanzania,
·
Meneja wa Mradi
wa AGPAHI – Shinyanga & Simiyu,
·
Wafanyakazi wa
AGPAHI,
·
Walezi wa Watoto,
·
Wadau mbalimbali
wa Afya na Haki za Watoto, (MDH, ICAP, JHPIEGO, Red Cross, World Vision Kagera,
HUYAWA (Huduma ya Watoto), Tumaini Children Centre, Uyacho Orphanage Centre,
TADEPA na TACDEN)
·
Watoto wa Kambi
ya Ariel,
·
Waandishi wa
Habari,
·
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Habarini
za asubuhi !
Ndugu
Mgeni rasmi, Awali ya yote napenda kutoa shukrani kwako kwa kuacha shughuli
zako na kuja kujumuika na sisi hapa kwenye Kambi ya Ariel (Ariel Camp).
Tunasema asante sana!
Pia
napenda kuwashukuru sana walezi waliokuja na watoto toka Simiyu na Shinyanga.
Vile vile napenda kuwashukuru wafanyakazi wenzangu wa AGPAHI na wadau wengine
kwa jitihada zao za hali na mali katika kuandaa kambi hii ya watoto. Hii ni
mara ya kwanza kwa AGPAHI kuandaa kambi hii katika mkoa wa Kagera, tunafarijika
sana kuwa hapa.
Ndugu
Mgeni rasmi, Shirika la AGPAHI ni shirika lisilo la kiserikali linaloendeshwa
na watanzania na watanzania wenyewe ndio sisi hapa.
Kuanzishwa kwa shirika linaloendeshwa na watanzania ilitokana na dira ya
serikali ya Tanzania na ile ya wafadhili yaani serikali ya Marekani
kutaka wazawa (serikali pamoja na mashirika yasiyo ya serikali) kuendesha
miradi mbalimbali inayoshughulikia masuala ya VVU na UKIMWI na masuala ya afya
ya mama na mtoto ili kuwa na miradi endelevu.
Shirika
letu linatoa huduma katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita. Huduma
zitolewazo ni pamoja na tiba na matunzo, kuzuia maambukizi ya virusi toka kwa
mama kwenda kwa mtoto na huduma za uzazi wa mpango. Hadi mwezi Machi mwaka huu, AGPAHI imeweza kuandikisha
wateja 96,638 (wanaume 34,342 na wanawake 55,975) kwenye huduma za matunzo ambapo 6,321 ni watoto walio
chini ya umri wa miaka 15 na hii sawa ni asilimia 7.
Vilevile AGPAHI imeweza
kuwaanzishia dawa wateja wapatao 63,048 (wanaume 21,555 na
wanawake 36,969) kwenye huduma za tiba ambapo watoto ni 4,524 ambayo
ni sawa na asilimia 7.
Dira
ya shirika ni kuhakikisha tunatokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa
watoto na kuondoa UKIMWI kwa watoto. Katika kutekeleza azma hiyo shughuli
mbalimbali zinatekelezwa ikiwa ni pamoja na kuwapatia watoto huduma za matunzo
na matibabu pamoja na huduma za kisaikolojia. Katika mikoa ya Shinyanga na
Simiyu, kuna jumla ya watoto 694,454 kati yao watoto 6,321 wanaishi na
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mgeni
Rasmi, shirika la AGPAHI lilianza huduma za malezi na kuwakutanisha watoto
katika vikundi vidogo vidogo baada tuu ya kuanzishwa kwake. Vikundi hivi vipo
katika vituo vya kutolea huduma za afya (yaani CTC) ambapo hadi sasa tuna jumla
ya vikundi vipatavyo 35 (vikundi 19 kwa mkoa wa Shinyanga na vikundi 16 kwa
mkoa wa Simiyu). Vikundi hivi vina jumla ya watoto 1,541.wanatoka
katika vituo mbalimbali kwenye halmashauri zote za mikoa ya Shinyanga na
Simiyu.
Katika
kipindi hiki cha wiki moja, watoto wameweza kujifunza mambo mbalimbali kama
vile: Usafi binafsi; Stadi za maisha na Mabadiliko ya tabia kutokana na msukumo
wa kundi; Taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI; Haki na wajibu watoto; Huduma na
msaada wa kisaikolojia; Jinsia, mahusiano ya kimapenzi na Uzazi wa Mpango;
Ufuasi mzuri wa dawa na Kuweka wazi hali yako (disclosure).
Katika
wiki hii ya kambi, watoto pia wameweza kupata huduma ya kisaikolojia pamoja na
kuhudumiwa na madaktari wa watoto kutoka Chama cha Madaktari wa Watoto
Tanzania.
Mbali
na mafunzo, watoto pia wamefanya matembezi na kuona mto Kagera, Kagera sugar
factory, kuona na kuelezewa maeneo ya vita vya IDD AMIN na pia wamefika
Mutukula (mpaka wa Tanzania na Uganda).
Ningependa
kutambua washindi wa Shindano la Mr and Miss Ariel camp ambalo lilifanyika jana
usiku. Washindi wetu walikua James Jackson (Mr. camp) kutoka Zahanati
ya Bugarama (MSALALA) na Anastazia Daniel
(Miss Camp) kutoka Hospitali ya Mkoa
wa Shinyanga. Naomba wasimame na tuwapigie makofi.
Ndugu
mgeni rasmi, napenda kutoa shukrani zetu kwa Watu wa Marekani kupitia shirika
lao la CDC ambao ndio wahisani wa kambi hii. Hata hivyo tuna
wafadhili wetu wengine kama EGPAF, UNFPA na USAID ambao nao wanatusaidia katika
kazi zetu. Pia shirika letu linafanya kazi kwa karibu sana na ofisi ya Waziri
Mkuu –TAMISEMI na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
ASANTENI
KWA KUNISIKILIZA!
LAUREAN
RUGAMBWA BWANAKUNU
Mgeni
Rasmi akikabidhi zawadi kwa watoto
Dr.Festo Manyama akipokea cheti cha ushiriki kutoka AGPAHI.
Dada Holo Bassu,mhudumu kutoka zahanati ya Itinje mara baada ya kupokea cheti cha ushiriki.Kaka Mbanga Kaijunga kutoka zahanati ya Negezi nae akipokea cheti chake cha ushiriki.
Zoezi la kukabidhi vyeti vya ushiriki likiendelea kwa Wahudumu kutoka katika vituo mbalimbali vya afya vinavyoshirikiana na shirika la AGPAHI.
Mwandishi Enjoy Mavuri kutoka kampuni ya The Guardian akipokea cheti cha ushiriki
Mama Grace Buberwa akitazama cheti chake cha ushiriki alichopewa na AGPAHI.
Wafanyakazi wa AGPAHI katika picha na mfanyakazi wa ELCT Hotel Bukoba (Aristides Musheshe)
Dada Liberator Kagenzi akiendelea na kazi
Dr.Haruna kutoka hospital ya mkoa nae alikuwa mmoja wa waalikwa.
Mwanahabari Irene Mark mbele ya Camera yetu.