Bukobawadau

MADAKTARI BINGWA KUTOKA 'USA' KUTUA HOSPITAL YA COSAD BUKOBA JUNE 7,2015

Madaktari bingwa wa magonja mbalimbali kutoka nchini Marekani wanatarajiwa kutoa huduma katika hospital ya COSAD iliyopo maeneo ya Nyamkazi ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba
 Prof Barr Brant  pichani kushoto ambaye ni mmoja wa Madaktari hao anayetoka  kwenye hospital ya Mayo Clinic,Minnesota Marekani  tayari amewasili mjini hapa kwa ajili ya shughuli maalum.
Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani (kulia) akitolea jambo ufafanuzi wakati akimkaribisha Prof Barr Brant anayetoka nchini Marekani  pichani kushoto.
Wataalam hao wa magonjwa  mbalimbali yya kina mama,watoto na wazee wanatalajia kuanzia kutoa huduma kuanzia tarehe 8.6.2015 hadi tarehe 4.7.2015 katika hospital CODAD ,hospital ya kisasa na yenye viwango
 Hakika Madaktari hao watakuwa msaada mkubwa hivyo wananchi nyote mnakaribishwa!!
 Waimbaji wa kikundi cha COSAD wakitoa burudani kwa wimbo maalum kwenye hafla fupi ya kumkaribisha Prof Barr Brant iliyofanyika Makao makuu ya COSAD maeneo ya Kibeta Bukoba
 Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani  katikati akiongoza Kikundi cha burudani wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Prof Barr Brant.
Pichani ni  Dr. Jessica Baitani na mwanae

Sehemu ya waalikwa katika hafla hiyo kushoto ni Mr. Mtusi wa Kagando Bukoba
Mdau unaombwa kumjulisha/kuwajulisha mwananchi mwenzako uwepo wa COSAD Clinic,Hospitali ambayo inatoa huduma ya juu katika  sekta ya afya kwa mawaziliano zaidi piga 0767 933  737
Wadau wakibadirishana mawazo
 COSAD Clinic ni Hospitali hiyo yenye vifaa vya kisasa inayotoa huduma kwa wagonjwa wa nje na ndani huduma inatolewa kila siku kuanzia saa 2 Asubuhi hadi saa 2 usiku/ jioni.
Next Post Previous Post
Bukobawadau