Bukobawadau

VIDEO/PICHA MAZISHI YA MAREHEMU GOSBERT RUSHEKYA GASPARY KIJIJINI GERA -MISSENYE

Mamia ya Wananchi na wakazi wa Gera Wilayani Missenye wameshiriki katika Shughuli ya mazishi ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary yaliyofanyika Jana nyumbani kwake Kijijini Gera
Msafara mkubwa wa watu ukielekea Kanisani kushiriki Ibada ya mazishi ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary.
 PITIA SEHEMU YA VIDEO MISA NA SHUGHULI YA MAZISHI HAPA CHINI Endelea kwa matukio ya picha kupata taswira kamili
Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary alipatwa na mautu usiku wa Ijumaa  juma lililopita baada ya kuvamiwa na watu wasiojulika na kumjeruhi na vitu vyenye ncha kali, tukio linalo husishwa na mauaji ya kukata watu makoromeo,(Mauaji yanayo zidi kutishia amani mkoani Kagera.)

 Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary alipata Majeraha makubwa sehemu za Kichwani na Shingoni yaliyo sababisha kuvuja damu nyingi kabla ya mauti kumkuta alfajiri ya Tarehe 20 ,2015 Kama ilivyoripotiwa na Mtandao wa Bukobawadau.


 Fr. Godwin Rugambwa wa Kanisa Katoliki parokia ya Mugana akiongoza Ibada ya mazishi hayo

 Wanakwaya wakiendelea na Ibada ya maziko ya Marehemu Gosbert Rushekya K. Gaspary

Mamia ya Waumini wakiendelea kushiriki Ibada ya mazishi ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary.

  Wakati shughuli ya Ibada ikiendelea

Majonzi makubwa kwa  Mjane wa Marehemu pichani kushoto na Dada wa Marehemu (kulia)

 Wanafamilia wakikabiliana na majonzi ya mpendwa wao, aliyekuwa mpigania Imani na mwenye msimamo asiye yumba katika kutetea Imani na msimamo wa kanisa katoriki.

 Pichani anaonekana Bwana Henry Bitegeko mwenyekiti wa Kigango Gera

Familia ya marehemu kupitia Bukobawadau inatoa shukrani kwa wote walioshiriki Mazishi haya,mwenyezi mungu awazidishie moyo wa upendo na mshikamano katika Imani, inawaomba kuendelea kuwaombe hasa katika kipindi hiki kigumu.

Baadhi ya watu  waliojitokeza kushiriki mazishi haya yaliofanyika Kijijini Gera Missenye.

 BUKOBAWADAU BOG tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241

Taswira mbalimbali Ibada ya mazisha ikiwa inaendelea

Hakika inahuzunisha sana 

 Kifo hiki kimetokana na watu wenye tamaa wanaotakiwa kulaaniwa vikali kwa kitendo hiki cha kinyama

 Poleni sana wanafamilia,mola akupeni moyo wa subira na kuweza kuyashinda majaribu

 Baadhi ya waombolezaji kama wanavyo onekana katika hali ya Simanzi kubwa.

 Bwana Nelson Rwiza mmoja wa waombolezaji.

 Dada wa Marehemu, na Mama mzazi wa Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary

Wanafamilia  wanaata fursa ya mwisho kutoa heshima zao za mwisho kwa mpendwa wao.

 Mama G mara baada ya kutoa heshima zake za mwisho

Kiongozi wa Jumuiya akitolea jambo ufafanuzi

 Salamu za rambirambi kutoka chama kikuu cha ushirika Kagera KCU

Mwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Nkenge Bi. Asumpter Nshunju Mshama

 Bw. kadogo  mwakilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

 Salaam za rambirambi zikiendelea kutoka katika makundi mbalimbali

 Mkuu wa Shule ya SekondariMkuu wa shule ya Kadea , inayomilikiwa na Chama cha Maendeleo ya Kanyigo (Kadea) akitoa salaam na kukabidhi rambirambi kwa familia

 Nao wanafunzi wanafikisha rambirambi zao.

 Rambirambi kutoka katika familia ya Lwamgira

Historia ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary inaonyesha katika uhai wake aliwahi kuwa mwenyekiti wa kikundi cha MAYAWA kwa Vijiji vya Gera-Ishozi na Ishunju,Karani wa  kituo cha mazao Gera,mjumbe wa bodi ya sekondari Gera, muhasibu wa Parish ya Gera na mhasibu msaidizi wa Parokia na mhasibu wa kamati ya Upadrisho.

Kwa niaba ya Ndg Roman Lwamgira, Domina  Lwamgira,Francisca na Alistides Lwamgira bahasha ya rambirambi inakabidhiwa kwa familia ya MarehemuGosbert Rushekya Kamugisha Gaspary

 Baadhi ya waombolezaji walihudhuria mazishi hayo ikiwemo viongozi wa Kimira ,wanasiasa na maofisa mbalimbali.

Umati wa watu ukielea eneo la kaburi mara baada ya kushiriki Ibada.

 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary likiingizwa Kaburini.

 Baba Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mugana akiweka udongo kaburini

Zoezi la kuweka Udongo kaburini likiendelea

Wanafamilia wakiweka Udongo kaburini.

 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika Mazishi ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary

Marehemu ameache Mjane na watoto watano,wakiume wawili na wakike watatu

Waombolezaji wakiweka udongo kaburini

 Willy Bukobatours Rutta na sehemu ya waombolezaji pichani

 Simanzi kubwa kwa watoto na marehemu na wanafamilia

 Wadau mbalimbali walioweza kuhudhuria mazishi ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugesha.

 Hakika ni simanzi kubwa kama inavyo onekana kupitia picha na sehemu ya Video mwisho wa ukurasa huu.

Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kushiriki mazishi haya

Fr Traseos Lutajama ,Paroko wa Ishozi akishirikiana na Fr Medard na Fr. Bahainako wa mugana kwa pamoja wamewahasa waumini kurudi katika misingi ya malezi na maadiri

 Kila mtu akionyesha kuguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine

 Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu Gosbert Rushekya Gaspary  mahali pema peponi,

Muendelezo wa picha  takribani 200 na taarifa nyinginezo zaidi jiunge nasi katika ukurasa wetu wa facebook na  kumbuka Ku'Like' ukurasa huo kupitia link hii BUKOBAWADAU MEDIA

Mmoja wa waombolezaji kwenye mazishi ya Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary.

Kwa matukio ya picha zaidi ya 100 Ingia kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya link hii>>>BUKOBAWADAU MEDIA

 Ndugu Rameck Rushekya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Kaka yake mpendwa.

 Sehemu ya wanafamilia wakiweka mishumua kwenye kaburi la mpendwa wao Marehemu
Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary



Omwami kazi Apolonia Lutinwa  wakati akiweka mshumaa kwenye kaburi.

 Utaratibu wa kuweka mishumaa ukiendelea.

Marehemu Gosbert Rushekya Kamugisha Gaspary alizaliwa TAREHE 4.6.1964 na kupata elimu yake ya msingi shule ya msingi Gera alipohitimu darasa la saba mwaka 1980

Taswira mbalimbali mazishi yakiendelea

 Wanafamilia wakiweka mishumaa.

 Matukio mbalimbili eneo la kaburi

 Mumimu kupitia sehemu ya Video iliyopo chini kabisa mwisho wa ukurasa huu.

 Bukobawadau Blog tunatoa pole kwa wafiwa wote

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe amen! R.I.P Mpendwa wetu.
 Wasifu wa Marehemu ukisomwa na Bw. Elphace Rwezaula
 Hali ya simanzi na vilio kutoka kwa waombolezaji
  Huu ndiyo mwisho wa safari ya maisha ya Mendwa wetu Gosbert Rushekya.
 Kutoka maeneo ya Kashai Mjini Bukoba wanaonekana wadau walioweza kushiriki mazishi haya.
 Omwami kazi Apolonia Lutinwa  pichani
 BUKOBAWADAU BOG tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
....TAZAMA SEHEMU YA VIDEO HAPACHINI...
Kwa matukio ya picha zaidi ya 200 Ingia kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa kubofya link hii>>>BUKOBAWADAU MEDIA
Next Post Previous Post
Bukobawadau