Bukobawadau

HAFLA YA ROTARY CLUB BUKOBA YAFANA

Baadhi ya Wajumbe wa Rotary Club Bukoba wakisalimiana na Mkurugenzi Fiosmin Hotel Bi Lilian Rwakatare,walipowasili kushiriki hafla ya Rotary Club iliyofanyika katika hotel hiyo siku ya jana July 4,2015.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika eneo la wazi katika mazingira ya Fiosmin hotel iliyopo barabara ya Kashura Mjini Bukoba.
 Rotn.Peace Kabyemera akiwapungia mkono waalikwa waliofika  katika hafla hiyo
 Kushoto ni Rtn. Eunias Ntangeki ambaye ndiye Rais mpya wa Rotary Club Bukoba, akisalimiana na Rais wa COSAD Tanzani Ndg Smart Baitani ambaye pia ni mjumbe wa Rotary Club Bukoba.
 Wajumbe wa Rotary Club Bukoba wakibadilisha mawazo ,mapema kabla ya hafla hii kuanza rasmi, ROTARY CLUB BUKOBA ni Klabu inajishughulisha na miradi mbalimbali katika kutoa huduma kwa kuimarisha miundombinu ya Elimu,usafi ,afya na shughuli nyingine za kiuchumi katika kuleta maendeleo ya jamii na kupunguza umasikini kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera
Rais mpya wa Rotary Club , Dr Eunias Ntangeki pichani katikati,baada ya kukabidhiwa rasmi nafsi hiyo kutoka kwa  Rotarian Bw. Archard Ngemela pichani kulia ambaye sasa ni Rais mstaafu.
Rotary Club Buboka wanayo furaha na kujivunia kwamba kupitia jitihada za pamoja kati ya jamii, wana Rotary wa kitaifa na kimataifa, taasisi zisizo za kiserikali, jamii ya kitabibu na makampuni ya kibiashara wameweza kufanya mambo makubwa kama ilivyo ainishwa hapo awali kupitia machapisho mbalimbali na nyeshwa yalioonyeshwa kwenye Projecta wakati hafla hii ikiendelea..
Rtn.Archard Ngemela akitolea ufafanuzi mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha Uongozi wake.
 Rais Mpya wa Rotary Club Bw. Eunis Ntangeki akiwatambuliza viungozi wapya wa Rotary Club Bukoba 2015-2016
 Rais wa COSAD Tanzani Rtn. Smart Baitani akitolea jambo ufafanuzi
Rotn.Bw.Joas Masasi pichani kulia akimuapisha Ms happiness essau kuwa Mjumbe mpya wa Rotary Club Bukoba
 Sasa ni Rotarian Ms. Happiness Essau mara baada ya kuapishwa.
 Katika picha maalumu kwa ajili ya kumbukumbu kupia Bukobawadau Media.
 Rotarian Ibra anamtambulisha Bi Brigitte Karg kama mjumbe mpya wa Rotary Club Bukoba.
Bi Brigitte Kagr akipongezwa na Installation Officer wa Rotary Club Bukoba ,PAG  Mashasi mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe mpya.
 Pichani ni baadhi ya Wageni waalikwa .
Rtn. J.Lutabingwa katika meza na waalikwa wa hafla hiyo
Mr.Walter Rwey-Robert akiwa katika hafla hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella ,mgeni rasmi akiongea na wadau walioshiriki katika hafla hiyo
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mh.John Mogella akitoa neno katika hafla hiyo na kuwapongeza Rotary Club Bukoba kwa jinsi wanavyo changia katika shughuli mbalimbali kijamii.
 Mdau kutoka kiwanda cha Tanica akitoa mchango wake kuichangia Klabu ya Rotary Bukoba
 Katika kuendeleza ushirikiano kwenye maswala ya jamii,naye Mkurugenzi Fiosmin Hotel Bi Lilian Rwakatare anapata kutoa mchango wake
 Kwa kutambua umuhimu wa huduma katia jamii,Mdau pichani anapata fursa ya kuchangia kiasi cha shilingi laki mbili
 Halambee ya kuchangia mfuko kupitia mnada wa bidhaa mbalimbali ikiendeshwa Mc muongozaji wa shughuli nzima Bw. Smart Baitani
 Picha ya Baraza la mawaziri la kwanza baada ya mapinduzi iliyonunuliwa kwa takribani dollar mia mbili na kuzawadiwa kwa Mgeni Rasmi katika hafla Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella.
 Kofia iliyotengenezwa kiasili  imeweza kununuliwa kwa dollar 100
 Mzee wetu pichani akiwa tayari kavaa kofia aliyo inunua kupitia mnada wa harambee ya kuchangia mfuko wa Rotary Club Bukoba
Waalikwa wakifuatilia kinacho endelea katika hafla hiyo.
 Dr. Jessica Baitani katika utambulisho
Rtn. Joas Rwegoshara muweka hadhina mkuu wa Rotary Club Bukoba akitoa tathmini
BUKOBAWADAU BOG tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu ,pia kwa taarifa au shughuli yotote kama kurusha habari na Covarage ya matukio kwa ajili ya kumbukumbu na ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043, 0715 505043 ,0768 397241,0673 505045
Baadhi ya waalikwa katika hafla hiyo
Baadhi ya Wajumbe wa Rotary Club Bukoba na waalikwa walioshiriki katika hafla  hiyo
 Mkurugenzi Fiosmin Hotel Bi Lilian Rwakatare akiteta jambo na Dr. Jessica Baitani.
 Muda wa kupata musosi.
Utaratibu wa kupata msosi safi ulio andaliwa na kampuni ya Mwanamama Rtn. Godliver Bayona
 Mzee wetu Rtn. J. Lutabingwa akipata huduma ya Chakula
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella akibadilishana mawazo na Rais wa COSAD Tanzani Rtn. Smart Baitani 
Rais wa Rotary Club Bukoba katika picha na  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella
Naye kijana Hussein anapata fursa ya kupata picha na Mh.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella katika picha ya kumbukumbu na Rais mstaafu wa Rotary Club Bukoba, Bw Archard Ngemela
Mmoja wa waalikwa pichani
Kwa mbali wanaonekana wadau pichani katika hili na lile 
Taswira  mbalimbali katika hafla hiyo
Mr. Bube na Ms Brittany Leitch ambaye ni Afisa Mipango wa COSAD Tanzania .
Rtn. Godliver Bayona
Mkurugenzi Endeavour Group Ltd (kiwanda cha kutengeneza nguo Bukoba)
 Kwa matukio ya picha zaidi ya 200 zinapatikana katika Ukurasa wetu wa facebook, Unaweza kujiunga nasi kupitia au kugonga link hii >>> BUKOBAWADAU JULY 2015
Wanaonekana waalikwa wakifuatilia mtiririko wa ratiba ya hafla hii maarufu kama (Rotary Club of Bukoba-Istalation Evening)
 Pichani  Mr Walter Rwey-Robert wakati akitoa mchango wake.
MWISHO BUKOBAWADAU BOG TUNAENDELEA KUKU KUMBUMBUSHA KUWA;tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu ,pia kwa taarifa au shughuli yotote kama kurusha habari na Covarage ya matukio kwa ajili ya kumbukumbu na ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043, 0715 505043 ,0768 397241,0673 505045
Email:bukobawadau@gmail.com
Insta:@bukobawadau
Picha zaidi ya 200 zinapatikana katika Ukurasa wetu wa facebook, Unaweza kujiunga nasi kupitia au kugonga link hii >>> BUKOBAWADAU JULY 2015
Next Post Previous Post
Bukobawadau