Bukobawadau

INASEMEKANA WAWILI WAPIGWA RISASI ZANZIBAR

 Watu wawili wanadaiwa kupigwa risasi na mmoja kujeruhiwa vibaya huko Makunduchi kwenye uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. Kheri Makame Hassan (42) na Ramadhan Hijja Hassan (29) Ali Seif Issa (38). Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Unguja Juma Saadi amesema hana taarifa za watu kupigwa risasi na taarifa alonazo ni kwamba risasi imepigwa juu kwa bahati mbaya.
Dk Seif Suleiman wa Hospitali wa Al Rahma amethibitisha kupokea majeruhi na amesema anasubiri picha za X Ray ili kujua majeraha hayo yametokana na nini lakini katika uchunguzi wa awali umeonesha kuwa majeraha hayo huenda ikawa ni risasi kutokana na kuwacha uwazi katika miili yao. Hadi sasa majeruhi hao wamelezwa hospitali ya Al Rahma wakipatiwa matibabu ambapo mmoja hali yake ni mbaya.
 Kama tulivyo ipokea kutoka vyanzo mbalimbali
Next Post Previous Post
Bukobawadau