Bukobawadau

KIJANA ASHRAPH KYOBYA 'MOTOTO WA IBWERA' MWENYE NDOTO YA KUWA MWANASIASA HODARI

Pichani ni Kijana  Ashraph Sadru Kyobya ,anayevutiwa kuwa mwanasiasa,Ni mzaliwa wa kijiji cha Ibwera Kati Wilaya ya Bukoba Vijijini ni kijana msomi  aliyepata elimu ya juu ngazi mwenye shahada ya sayansi ya jamii katika masuala ya kielimu na shahada ya pili  ya utawala katika masuala ya kibiashara (masters of business administration),katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 

Kufanikiwa ni ndoto ya kila mmoja wetu, hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuwa na mawazo chanya, Kwa sasa Kijana Ashraphanajishughulisha kama Meneja Masoko wa Kampuni iitwayo TRAVELPORT (T) LTD iliyopo jijini Dar es Salaam ,Akiongea na Bukobawadau Media amesema;''Kwa muda mrefu nimetamani kuwa mwanasiasa nikiwa na lengo la kuwawakilisha wananchi wenzangu  katika fursa mbalimbali ''
 Akimnukuu mwanafalsafa mahiri aitwae PLATO ,Kijana Ashraph anasema 'wale wenye weledi, mahiri na waadilifu wasiopenda siasa hujikuta wakitawaliwa na watu wa hovyo. Hivyo yeye ni mmoja kati ya walio weledi na waadilifu'

Tunawatakia usiku mwema!

Next Post Previous Post
Bukobawadau