Bukobawadau

MITAZAMO MBALI MBALI JUKWAANI

Tuachane uroho wa madaraka kwa kuwadanga na kuwahadaa wananchi. Leo tunawaonyesha wezi na kuwafikisha mahabusu halafu kesho tunakula nao na kuwasifia kwa kazi zao. Wengine wanasema ety ana wafuasi wengi, hivi tunataka kushika madaraka au tunataka kuwa na serikali bora itakayolinda na kutetea maslahi ya wananchi???

Lusifa ana wafuasi wengi sana hapa duniani hata kufikia hatua ya kumjaribu Mungu lakini kamwe Mungu hakuwai kumfikiria kumrejesha Lucifa kuwa malaika wa sifa kama alivyokuwa awali, Nitakuwa wa mwisho kuunga mkono usanii na udanganyifu wa kisiasa unaotaka kutokea ndani ya nchi yangu.
By Mesaya
 #‎HABARI‬ LOWASSA AKARIBISHWA RASMI UKAWA
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema umemkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa kujiunga nao katika harakati za kuking'oa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mbatia: Tunamkaribisha rasmi aliyekuwa waziri mkuu mstaafu, Edward Ngoyaye Lowasa kujiunga na UKAWA, ni mchapakazi makini na mtekelezaji wa majukumu, UKAWA ndio tumaini la Tanzania, tusikubali kunyamaza pale ambapo sauti zetu zinazimwa kwa lazima. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA, UKAWA ndio tumaini letu.
Mbatia: Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri
Lipumba: "Lowasa alishasema yeyote mwenye ushahidi aulete..hapa tumekaribisha Watanzania wote kujiunga. Kuhusu CUF kusuasua UKAWA: Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakaechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.
Next Post Previous Post
Bukobawadau